You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Sauti zetu
Vidio zetu
Yanayoangaziwa
Maandamano Kenya
Mzozo wa Israel na Hamas
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani
Matangazo
Picha: Zoonar/picture alliance
Picha: Zoonar/picture alliance
Makala zetu
Sikiliza makala kemkem tulizokuandalia
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Sema Uvume: Programu inayosaidia wasioona kutumia mitandao
Programu maalum za kuwasaidia wenye ulemavu wa macho kutumia majukwaa hayo zimeanza kufanya kazi.
Joto kali lina athari gani mwilini ?
Daktari Jalab Ashraf atowa maelezo zaidi jinsi ya kuhakikisha tunabakia imara kiafya katika kipindi hiki cha joto kali.
24.03.2024 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa yaliyomo ni Taarifa ya habari za ulimwengu na makala zetu ikiwa ni pamoja na Maoni mbele ya meza ya duara.
Binadamu apandikizwa figo ya nguruwe kwa mara ya kwanza
Figo hiyo ya nguruwe ilibadilishwa vinasaba na kuondolewa kwa jeni zenye madhara kwa mpokeaji.
Tabia za vijana wakati wa miezi ya toba
Lilian Mtono anazungumza na vijaa haswa kuhusu kubadilisha mienendo ya kimaisha, wakiachana na maovu, kuwa watii, wanyenyekevu na kufanya ibada zaidi. Lakini ni kwa bahati mbaya kwamba wengi hurejea kwenye mienendo ileile ya kimaisha ya kabla ya kipindi kama hiki cha toba.
Hali ya makazi mijini Afrika Mashariki
Kwenye Makala Yetu Leo, tunaangazia hali ya makazi katika miji kwenye ukanda wa Afrika Mashariki. Shirika la makazi la Umoja wa Mataifa, UN-Habitat, linasema idadi ya wakazi wa mitaa ya mabanda inatazamiwa kufikia bilioni 3 ifikapo mwaka 2050 huku mzozo wa makazi ukizidi kuwa mkali duniani.
Mchakato wa uraia wa nchi mbili
Mara hii tunazungumzia juu ya hatua iliyochukuliwa na bunge la Ujerumani ya kuidhinisha taratibu za kuurahisisha mchakato wa mhamiaji kupatiwa uraia wa Ujerumani na wakati huo huo kuendelea na uraia wa nchi yake ya uzawa, kwa kifupi, mchakato wa uraia wa nchi mbili.
Madhila waliopitia watu wa Mariupol
Ripoti ya shirika la Human Rights Watch, inabaini kwamba huenda kulifanyika huko Mariupol vitendo vya uhalifu wa kivita.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani- Sehemu ya Nne
Mara hii tunamulika mauaji ya kimbari yaliyofanywa na serikali ya ukoloni wa Wajerumani kati ya mwaka 1904 hadi 1908 dhidi ya makabila ya Herero na Nama huko Nambia, Kusini mwa Afrika.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani- Sehemu ya Tatu
Sikiliza sehemu hii ya tatu ya mfululizo wa makala zetu juu ya ukoloni barani Afrika.
Huduma za serikali ya Zanzibar mtandaoni
Mwandishi wa DW Salma Said anazungumza na Mkurugenzi mtendaji wa serikali mtandao kutoka Zanzibar, kuhusu uendeshaji wa shughuli za serikali na huduma kwa njia ya mtandao. Kufahamu mengi sikiliza mahojiano kamili.
Nafasi ya chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania
Rashid Chilumba anaongoza kipindi cha Maoni kutathmini nafasi ya chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania.
Kauli ya Papa Francis yazua hisia mseto
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema katika mahojiano kwamba Ukraine inapaswa kuwa na kile alichokiita ujasiri wa kupeperusha "bendera nyeupe" kama ishara ya kusalimu amri na kukubali kufanya mazungumzo ya kumaliza vita na Urusi. Kauli hiyo imeichukiza mno Ukraine na washirika wake wa Magharibi.
Uraibu wa mihadarati- Jinsi ya kuachana nao
Je ulijua kuwa heroini ni dawa ya kulevya ya tatu miongoni mwa mihadarati inayotumika zaidi kinyume cha sheria Tanzania?
Madhara ya kiafya kwa madereva wa bodaboda
Makala ya afya yako Deo Kaji Makomba kutoka makao makuu ya Tanzania, Dodoma, anaangazia madhara ya kiafya wanayoweza kuyapata madereva wa pikipiki maarufu kama boda boda ambao hujishughulisha na shughuli za usafirishaji abiria katika maeneo mbalimbali nchini humo.
Usiweke simu yako kwenye mchele mkavu
Katika Sema Uvume wiki hii Suleman Mwiru anatizama tahadhari iliyotolewa na kampuni ya Apple juu ya tabia ya kuziweka simu kwenye mchele mkavu pindi zinapodondoka kwenye maji, badala yake fanya yafuatayo.
Zitto Kabwe amekiachaje chama cha ACT-Wazalendo ?
Silikiza mahojiano ya mwanasiasa wa upinzani Tanzania Zitto Kabwe na George Njogopa wa DW-Kiswahili kwenye Kinagaubaga.
Somalia yajiunga rasmi na EAC
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imeikaribisha rasmi Somalia kuwa mwanachama wake mpya.
Kaiko Njike: Waasi bado wanatatiza raia mashariki ya Kongo
Sudi Mnette anazungumza na Kanali Kaiko Njike, msemaji wa jeshi la Kongo linalopambana na waasi mashariki ya nchi hiyo.
Mastaa wageuka ombaomba mitandaoni?
Ni jambo la kawaida kuona ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa mastaa wakiomba msaada wa kifedha kutoka kwa mashabiki wao na wafuasi wao. Iwe ni kwa ajili ya kulipa bili za matibabu, kulipa kodi za nyumba au hata kununua kitu cha thamani. Bruce Amani anaimulika mada hii katika Vijana mchakamchaka.
Ukraine inataka kuungwa mkono na Waafrika
Ukraine inatafuta uungwaji mkono kutoka katika pande tofauti za ulimwengu kufuatia vita vyake a Urusi. Hivi karibuni ili kulifanyika kongamano la kimataifa kuhusu vita hivyo lililofahamika kama Cafe Kyiv, mwandishi wa habari Issac Amuke kutoka Kenya alikuwa mwana jopo katika kongamano hilo lililofanyika Februari 2024. Zaidi msikilize alipozugumza na Sudi Mnette.
Juhudi za serikali ya Kenya kuzalisha dawa zake yenyewe
Ungana na Wakio Mbogho, Ripota wa DW mjini Nakuru, Kenya, katika Makala ya Afya Yako inayomulika jitihada za taifa la Kenya kustawisha uzalishaji wa dawa na bidhaa za matibabu nchini humo.
Biteko:Uhakika mgao wa umeme mwisho Machi Tanzania
Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania, Dotto Biteko amesema taarifa ya kuufikisha mwisho kwa mgao wa umeme Tanzania mwezi Machi.
Kenya yakabiliana na saratani ya mlango wa kizazi
Kukabili matatizo ya mimba kuharibika na mtoto kufa tumboni
Je afrika inawezaje kuondokana mgogoro wa umeme wa uhakika?
Afrika ina vyanzo vingi vya nishati mbadala ambavyo vinaweza kulipatia bara hilo nishati ya kutosha na ya uhakika. Hata hivyo, pamoja na utajiri huo, takribani watu milioni 600 kati ya watu bilioni 1.4 barani humo wanakosa huduma ya uhakika ya umeme. Katika vijana mubashara leo tunakuuliza kijana, je afrika inawezaje kuondokana na kadhia hiyo ya ukosefu wa umeme wa uhakika?
Je umeshawahi kuwa kwenye mahusiano na mtu aliyekuzidi umri?
Kuna mitazamo tofauti juu ya vijana wanaojihusisha na uhusiano wa kimapenzi na watu waliowazidi umri. Lakini vipi mahusiano hayo yanapogeuka kuwa ya kusaka maslahi? Suleiman Mwiru anakueleza zaidi katika Makala hii.
Vijana Mchakamchaka: Je, unaitumiaje simu yako?
Je, wewe unaitumiaje simu yako? Ungana na Selina Mdemu akizungumzia matumizi ya simu kwa vijana.
Wimbi la rekodi za dunia za Guinness
Katika Makala hii ya vijana mchakamchaka, tunafahamu zaidi kuhusu rekodi za dunia, za Guinness. Je, ni za kujipatia sifa tu? Au zinakuza maadili ya kijamii na kuhamasisha jamii kuhusu masuala muhimu? Ni rekodi ipi ambayo ungependa iandikwe?
Kujiuzulu kwa Rais wa Hungary K. Novak
Jumamosi ya Februari 10, 2024- Rais wa Hungary Katalin Novak alitangaza uamuzi wake wa kujiuzulu kufuatia uamuzi wa kutoa msamaha kwa mtu aliyekuwa jela kwa kosa la kukutwa na hatia ya kuficha taarifa muhimu kwenye kesi ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto. Katika kipindi cha Mwangaza wa Ulaya, tunaangazia sakata hili lililomfanya Rais Novak, rais wa kwanza mwanake wa Hungary kujiuzulu.
Unapendelea kocha wa Kiafrika au wa kigeni?
“Kama makocha wa Kiafrika watapewa raslimali za kutosha na uhuru wa kufanya kazi yao bila uingiliwaji, hakuna timu ya taifa barani Afrika itahitaji kocha wa kigeni.“ Unakubaliana na hii? Hiyo ndio mada yetu katika Vijana Mubashara.
Wimbii la migomo: Ujerumani yakabiliwa na mkwamo
Mwaka mpya ulianza kwa wimbi la migomo nchini Ujerumani. je, Wajerumani wanagoma zaidi hivi sasa kuliko hapo kabla na je, nchi hiyo inakabiliwa na tishio la hali kama ya nchini Ubelgiji au Ufaransa?
Sheria mpya za uchaguzi nchini Tanzania
Zainab Aziz amewakaribisha mezani wachambuzi kuzungumzia sheria mpya za uchaguzi nchini Tanzania. Sikiliza mjadala huo.
Madhara ya kusitisha ufadhili kwa UNRWA
Mohammed Khelef anachambua athari mbaya za uamuzi wa kusitisha ufadhili kwa shirika la UNRWA.
Joseph Butiku na tathmini ya miaka 47 ya CCM
Joseph Butiku na tathmini ya miaka 47 ya tangu kuzaliwa kwa CCM, chama tawala cha Tanzania.
Mwangaza wa Ulaya: Ulaya imejiandaaje kwa kurejea utawala wa Donald Trump?
Wakati kampeni za urais nchini Marekani zikiashiria uwezekano wa kurudiwa kwa mchuano kati ya Donald Trump na Joe Biden, Ulaya inafuatilia kwa wasiwasi mkubwa. Siyo tu kura za uchunguzi wa maoni zinazompa Trump nafasi halisi ya kurejea Ikulu ya White House. Gazeti la New York Times liliripoti kuwa viongozi wengi wa dunia wanaamini Trump anarudi kwa muhula wa pili. Zaidi katika Mwangaza wa Ulaya.
Kinagaubaga: Mwelekeo wa soka nchini Tanzania
Kocha Matola : Soka la Tanzania bado lina changamoto kubwa. Tanzania ilifungwa mechi moja na kutoka sare mbili AFCON.
Upopulisti, mitandao na demokrasia
Baruani Mshale anafafanua jinsi upopulisti unavyoshika kasi barani Afrika na jinsi zilivyo hatari kwa demokrasia.
Kinagaubaga: Kenya, Tanzania na Uganda kuandaa AFCON 2027
Rais wa shirikisho la soka la mpira wa mguu Tanzania TFF Wallace Karia aelezea nafasi ya Tanzania AFCON 2027.
Kinagaubaga: Mwamko wa kibiashara visiwani Zanzibar
Upi mwelekeo wa sekta ya biashara visiwani Zanzibar? Waziri mwenye dhamana Omar Said Shaban anaeleza kwenye Kinagaubaga.
Kinagaubaga: DP World yazidi kukosolewa Tanzania
Mjadala wa ubinafsishaji wa Bandari kuu ya Dar es Salaam kwa kampuni ya Dubai ya DP world umezusha wasiwasi kwa raia wa taifa hilo na kuanza kuwagawa watu kwa itikadi na maeneo wanayotokea.
Ugunduzi wa aina mpya ya Mbu na kitisho cha Malaria Kenya
Taasisi ya utafiti wa matibabu KEMRI imegundua aina mpya ya mbu nchini Kenya na imetoa tahadhari juu ya mbu hao hatari.
Vijana Mchakamchaka: Mtindo wa upigaji picha za kuvutia
Vijana Mubashara inaangazia umuhimu wa kupiga picha na jinsi vijana wa kileo walivyobadilisha tasnia ya upigaji picha.
Vijana Mchakamchaka: Nidhamu ya kufanya mazoezi
Sio wote wanaofanya mazoezi wana nia ya kujenga mwili. Vijana Mchakamchaka leo inaangazia sababu za vijana kuingia gym.
Vijana Mubashara: Sababu zinazokufanya usifikie malengo yako
Miongoni mwa sababu za mtu kutofikia malengo yake ni kupishana kiimani, kutilia mashaka uweko wako na kukatishwa tamaa.
Mbiu ya Mnyonge: Askari polisi na vitendo vya kikatili
Raia anatakiwa ajihisi yuko salama zaidi mbele ya maafisa wa polisi, lakini katika matukio kadhaa inakuwa kinyume chake.
Afya Yako: Umuhimu wa kufanya vipimo mara kwa mara
Kwenye Afya Yako leo, Selina Mdemu anazungumzia umuhimu wa kufanya vipimo vya mwili mara kwa mara ili kuchunga afya.
Dunia Yetu Leo Mchana Januari 20, 2024
Sikiliza Matangazo ya Mchana Januari 20, 2024 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.
Uteuzi wa Gabriel Attal kama Waziri Mkuu wa Ufaransa
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alimteua Januari 9 mwaka 2024, Gabriel Attal kuwa Waziri Mkuu mpya. Attal mwenye umri wa miaka 34 anachukua nafasi ya Elisabeth Borne aliyejiuzulu sambamba na serikali aliyokuwa akiiongoza. Hatua hii ya Macron inachukuliwa kama ya kimkakati na yenye lengo la kuisafisha serikali yake ambayo imekuwa ikikabiliwa na kashfa mbalimbali.
Kinagaubaga: Lazima wakazi wote waondoke Ngorongoro
Mpango wa kuwahamisha jamii ya wamasai katika Hifadhi ya Ngorongoro Tanzania, umeendelea kukabiliwa na ukosoaji huku, makundi ya watetezi yakilalamika kuwa serikali inazuia huduma muhimu kwa lengo la kuwashinikiza waondoke.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 3 wa 4
Ukurasa unaofuatia