You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Sauti zetu
Vidio zetu
Yanayoangaziwa
Maandamano Kenya
Mzozo wa Israel na Hamas
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani
Matangazo
Picha: Zoonar/picture alliance
Picha: Zoonar/picture alliance
Makala zetu
Sikiliza makala kemkem tulizokuandalia
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Masharti yapunguzwa kwa wanaotafuta kazi Germany
Mnamo Juni Mosi Ujerumani ilianza kutumia rasmi sheria mpya ambayo inawaruhusu watu wenye ujuzi kutoka mataifa ambayo hayapo ndani ya Umoja wa Ulaya, kuingia nchini humo na kutafuta ajira. Sheria ambayo inatajwa kuwa itapunguza changamoto ya uhaba wa wafanyakazi katika kada mbalimbali kwenye taifa hilo la Ulaya.
Magauni ya harusi kuchanganywa na vitambaa vya rangi
Mara nyingi tumezoea bibi harusi kuvaa gauni jeupe, lakini wabunifu wa kiafrika wamekuja na ubunifu mpya wa kuchanganya vitambaa vya kijadi na vile vyeupe. Mwanamitindo Augustina Avonsige aliamua kuchanganya vazi la kienyeji la Ghana kente katika vazi jeope la harusi.
Uvaaji wa kofia za Kiyoruba na maana yake
Kofia za Kiyoruba zina utambulisho mpana katika utamaduni wa kabila hilo la Nigeria, kuanzia uvaaji wake na ushonwaji wake. Femi Adekambe amebobea katika ushonaji wa kofia za kitamaduni akizipa nakshi za kipekee. #77asilimia
Mapambo yanayotengenezwa kwa kutumia shanga
Mbali Mthethwa anafanyia kazi kuendeleza Sanaa ya mapambo ya shanga ambayo inazidi kufifia.
Watu wa nje ya Umoja wa Ulaya kufanya kazi Germany
Sura ya Ujerumani na Sheria mpya ya kuwaruhusu watu kutoka nje ya Umoja wa Ulaya kuja kufanya kazi Ujerumani.
Jukwaa la Manufaa
Angela Mdungu anakupa nafasi ya kutoa dukuduku pongezi, maoni au ushauri kuhusu masuala yanayohusu jamii inayokuzunguka.
Kinagaubaga: Athari za mradi wa SGR kwa watu wa Mombasa
Kadara Swaleh kutoka nchini Kenya anachambuwa athari za mradi wa reli ya SGR kwa wakaazi wa Mombasa.
Hedhi salama bado ni changamoto kwa wasichana
Hapo kabla ilikua ni nadra kulizungumzia suala la hedhi hadharani lakini muda inavyozidi mambo kuwekwa wazi hili linawapa nafasi wasicha kuzungumza suala hili kwa uwazi zaidi. #MsichanaJasiri
Kurunzi Live Hedhi Salama Day
Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya Hedhi Salama, bado wasichana na wanawake wengi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali wanapofikia kwenye siku hizo. Je kipi kifanyike kuwasaidia? Tizama video hii kisha utuambie.
Vijana na muenendo wa kujitoa wenyewe
Katika makala hii ya Vijana mchakamchaka, tunamulika muenendo wa kizazi maarufu cha Gen Z, wa kujitoa chenyewe bila wenza, au wapenzi. Kwa nini mtindo huu umeshika kasi sana? Nini kinawafanmya vijana kutaka kuwa na kile wanachoita “me time“ yaani kujitengea muda wao?
Miaka 75 ya katiba ya Ujerumani
Katiba ya Ujerumani iliyoundwa na kuanza kutumika Mei 23 mwaka 1949 sasa imetimiza miaka 75. Sikiliza hapa makala ya Sura ya Ujerumani inayoimulika katiba hiyo Kongwe.
Uganda yaanza kampeni ya chanjo dhidi ya homa ya manjano
Uganda imeanza tena kampeni ya kutoa chanjo ya homa ya manjano ili kuulinda umma dhidi ya ugonjwa unaosambazwa na mbu.
Mkutano wa mwaka wa WHO waanza Geneva
WHO yaangazia vipaumbele vya miaka minne ijayo baada ya janga la UVIKO-19.
Kwa nini wanaume wengi hawatafuti msaada wa afya ya akili ?
Katika mwezi huu wa kuhamasisha jamii kuhusu afya ya akili, swali linalozidi kuibuka ni: kwa nini wanaume wengi hawatafuti msaada wa afya ya akili? Kulingana na wataalamu wa saikolojia, inaonekana kuwa wanawake wengi wanagunduliwa na matatizo ya afya ya akili ikilinganishwa na wanaume. Lakini, ni nini hasa kinachosababisha tofauti hii ?
25.05.2024: Matangazo ya Mchana
Kwenye Matangazo ya Mchana utasikia pamoja na mengineyo taarifa ya habari za ulimwengu na makala ambazo ni pamoja na mjadala mrefu na wa kina wa Maoni kuhusiana na kifo cha ghafla cha aliyekuwa Rais wa Iran Ebrahim Raisi. Utasikia mengi kuhusu kiongozi huyo na kile kinachotarajiwa nchini humo baada ya kifo chake. Ungana nasi hapa.
Changamoto za mimba za utotoni
Kuwa mjamzito ukiwa kijana huweza kukuathiri vibaya.
Changamoto za mikopo midogomidogo
Mikopo ya haraka, mikopo poa inayotolewa na watu binafsi au taasisi ndogo za kifedha imekuwa tatizo kwa wafanyabiashara.
Rais wa Kenya William Ruto apendekeza kupandisha kodi
Zainab Aziz amewakaribisha mezani wachambuzi kuzungumzia mapendekezo ya kupandisha kodi nchini Kenya.
TCRA na usimamizi wa vituo vya habari Tanzania
Katika makala hii Mohammed Khelef ameketi chini na meneja wa huduma za utangazaji Andrew Kisaka kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA na kuzungumzia namna mamlaka hiyo inavyosimamia vyombo vya habari vya utangazaji Tanzania na hatua wanazozichukua pale vinapokiuka kanuni.
Namna akili ya kubuni AI inavyotumiwa kuwarubuni watu
Hapo awali matapeli walitumia ujumbe au barua pepe kufanya ulaghai lakini sasa wamegeukia teknolojia ya AI kutapeli.
Athari za mafuriko nchini Tanzania
Makala Yetu leo inaangalia athari zilizotokana na mvua kubwa zilizonyesha na kusababisha mafuriko makubwa Tanzania.
Ongezeko la mashambulizi dhidi ya wanasiasa Ujerumani
Kumekuwa na ongezeko la mashambulizi dhidi ya wanasiasa nchini Ujerumani. Wanasiasa hao wamekuwa wakikumbana na vipigo, matusi, kuchafuliwa na hata kutishiwa vifo.
Marafiki kupostiana mtandaoni siku ya "Birthday"
Utamaduni wa kusheherekea siku ya kuzaliwa umebadilika hasa katika zama hizi za kidigitali na kupostiwa mtandaoni.
Benin kitovu cha utalii barani Afrika
Je, umewahi kufikiria kuitembelea Benin? Nchi hii ndio chimbuko la dini ya Vodoo na tamasha kubwa la kila mwaka. Kuanzia jiji mahiri la Cotonou hadi kijiji kinachoelea majini cha Ganvie, 77 Asailimia inakupa sababu za kuitembelea Benin.
Wafungwa wanaosalia jela Burundi baada ya kumaliza vifungo
Ni kwa nini mfungwa asalie gerezani hata baada ya kumaliza kifungo chake? Ndilo swali ambalo makala ya Mbiu ya Mnyonge inaangazia kule nchini Burundi. Na je wanaofungwa kinyume cha sheria watapataje haki? Mtayarishaji wa makala ni Amida Issa akiwa mjini Bujumbura, Burundi.
Makamu wa Rais wa Zanzibar azungumzia umoja wa kitaifa
Wakati hatima ya ushiriki wa mshirika mdogo kwenye serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar, chama cha ACT Wazalendo, ikining'inia baina ya kubakia na kutoka, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa chama hicho, Othman Masoud Othman, anazungumza na Mohammed Khelef wa DW kuhusu uhalisia wa mambo ulivyo.
Nafasi ya Tanzania katika uwanja wa kidiplomasia
Katika Makala ya Kinagaubaga, Mwenzetu Florence Majani amezungumza na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa nchini Tanzania January Makamba, juu ya mambo mengi likiwemo hili la nafasi ya taifa hilo la Afrika Mashariki katika uwanja wa kidiplomasia.
Joel Nanauka katika Kinagaubaga na DW Kiswahili
Joel Nanauka kutoka Tanzania ni mwandishi wa vitabu na msomi aliyebobea katika masuala ya Diplomasia na uchumi na ni miongoni mwa vijana wenye ushawishi zaidi barani Afrika, kwa kuielimisha jamii hasa vijana kuhusu mambo yasiyofundishwa katika mfumo rasmi wa elimu ya darasani. Veronica Natalis amezungumza ne katika Kinagaubaga.
Vijana na ushiriki wao wa densi katika mitandao ya kijamii
Kama wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii bila shaka hivi karibuni utakuwa umekutana na vidio chungu nzima za vijana wakicheza aina mbalimbali za miziki. Mitandao ya kijamii kama vile YouTube, Tiktok, Facebook na Instagram sasa imegeuka kuwa jukwaa la vijana kuonyesha umahiri wao wa kucheza muziki. Nini kinasababisha vijana kushiriki densi hizo?
Nini kinafanya vijana kuvalia mavazi ya kupitiliza msibani?
Hapo kale taarifa ya msiba ilipokuwa ikiwafikia wengi, kubwa lililokuwa likiwajia vichwani ni kuhakikisha wanafika ulipo msiba na kutoa msaada wa kufariji wafiwa. Lakini sasa hali ni tofauti vijana wana namna yao ya kufika msibani, wakiwa wamevalia kweli kweli. Suali ni je nani yupo nyuma ya mtindo huu wa maisha kwa vijana wa sasa. Vijana Mchakamchaka inaangazia hilo. mtayarishaji ni Hawa Bihoga
Ujerumani yakabiliwa na uhaba mkubwa wa makazi
Uhaba wa makazi nchini Ujerumani, ni tatizo kubwa la kijamiii. Kupata nyumba ya kupanga hivi sasa limekuwa suala gumu ambalo linaweza kufananishwa na kushinda bahati nasibu. Ungana na Angela Mdungu katika makala ya Sura ya Ujerumani kufahamu zaidi kuhusu tatizo hilo.
Kukanda mwili: Faida na hasara zake
Ungana naye Angela Mdungu katika makala ya afya yako inayolitazama kwa kina suala zima la kukanda mwili, faida zake pamoja na athari za kiafya zinazoweza kumpata mtu kutokana na huduma hiyo.
Maumivu makali ya hedhi hudhibitiwaje?
Maumivu ya hedhi, wakati wa ngono, na matatizo ya usagaji chakula ni baadhi tu ya dalili zinazohusiana na endometriosis. Hali hiyo huathiri mwanamke mmoja kati ya kumi duniani kote. Ingawa kwa sasa hakuna tiba ya endometriosis, kuna njia za kuboresha maisha ya walioathirika. Katika mazungumzo haya ya dhati na Dk. Chinonso Egemba, Ritha anasimulia safari yake ya kupambana na ugonjwa huo.
Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania
Mohammed Khelef anaongoza Meza ya Duara kujadili miongo sita ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Blinken akumbusha "uwajibikaji" kati ya Marekani na China
Blinken yuko China akilenga kusaka suluhu ya masuala kadhaa yanayotishia utulivu wa kimahusiano baina ya mataifa hayo.
Mfumuko wa bei unavyobadili maisha ya wakazi wa Ulaya
Mfumuko wa bei bado unaendelea kushuhudiwa katika mataifa mengi duniani hususan barani Ulaya. Na hilo ndilo linalojadiliwa katika makala hii ya Mwangaza wa Ulaya.
WHO yasema dawa ya kikohozi ya J&J haipatikani tena Afrika
Dawa iliyogunduliwa kuwa na viambata vya sumu haipatikani tena katika nchi za Kiafrika ambako ilikuwa inauzwa.
Mikopo ya mitandaoni na chungu yake
Matangazo ya mikopo ya mitandaoni huwavutia watu kwasababu ya masharti yake nafuu. Lakini namna ya kudai madeni inatajwa kudhalilisha wadaiwa. Ungana na Florence Majani, katika makala yetu leo.
Je, umewahi kusikia kuhusu ''menopause'' ya wanaume ?
Inaweza kukushangaza kwamba wanaume nao huingia katika kipindi cha menopause. Tofauti na wanawake ambao menopause inaashiria kukoma kwa hedhi, wanaume nao hupatwa na andropause yani kukoma kwa uwezo wa kuzalisha.
Ujerumani kulifanyia mageuzi jeshi lake
Makala ya Sura ya Ujerumani leo inaangazia mpango wa Waziri wa Ulinzi Boris Pistorius wa kulifanyia marekebisho jeshi la nchi hiyo, "Bundeswehr". Maheuzi hayo yanatokana na kile anachokiita Pistorius kuwa kitisho cha kiusalama barani Ulaya.
Miaka 30 tangu mauaji ya Kimbari ya Rwanda
Rashid Chilumba anaongoza kipindi cha Maoni kujadili miaka 30 tangu kutokea mauaji ya kimbari nchini Rwanda.
Mwanamitindo wa Uganda anayetamba TikTok
Angella Summer Namubiru ni mwanamitindo kutoka Uganda, anaishi maisha ya kijijini na kujizolea umaarufu TikTok. Amekabiliwa na ubaguzi kutokana na rangi nyeusi ya Ngozi yake. Lakini sasa ameamua kutumia mitandao kuelemisha umma. #vijanamubashara
Umuhimu wa kocha na mkufunzi bora kwa mchezaji
Katika michezo, nafasi ya kwanza inamaanisha ubingwa. Mbali na talanta unahitaji washauri na wakufunzi bora watakao kuongoza kufikia ubingwa. Hawa huchangia ushindi nyuma ya pazia na kumsaidia mchezaji kuvikabili vikwazo na ukiritimba unaojitokeza katika safari ya mashindano. #vijanamubashara
Ipi sababu ya vijana kujiingiza katika magenge ya kihalifu?
Kuongezeka kwa magenge ya kihalifu ya vijana katika baadhi ya nchi barani afrika kumezidi kuibua wasiwasi. Makundi hayo ya kihalifu mara nyingi hufanya uporaji na kuwaumiza wananchi. Wengi wanasema hali ngumu ya kiuchumi ndio inachangia vijana kujitumbukiza katika magenge hayo. Sylvia Mwehozi ana mengi katika vijana Mubashara, 77asilimia
Unajuwa unaweza kununua bidhaa zako bila ya kwenda madukani?
Kupitia simu yako ya mkononi, au kompyuta, unaweza kununua bidhaa zako kwa urahisi na kuzipata kwa muda mfupi tu. Hizi zinaitwa biashara za mtandaoni. Ni aina ya biashara ambapo mteja na muuzaji hawaonani ana kwa ana bali kupitia mtandao. Tatu Karema anakufahamisha zaidi katika makala ya Vijana Mchakamchaka
06.04.2024: Matangazo ya Mchana
Matangazo ya Mchana, yanasikika hapa. Utasikia Taarifa ya Habari ambako kuna mengi yanayogonga vichwa vya habari duniani. Lakini pia kuna Maoni mbele ya Meza ya Duara, ambapo wafuatiliaji wanamchambua, Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na changamoto zinazomkabili. Karibu.
DR Congo yapata Waziri Mkuu Mwanamke
Je Rais Tshisekedi amemchagua Judith Suminwa Tuluka kwa sababu ni mtu wake wa karibu au ni kutokana na uwezo alionao?
Habineza na hali ya upinzani Rwanda
Frank Habineza anazungumza juu ya hali ya kisiasa katika taifa hilo dogo la Afrika Mashariki.
Ulaghai wa wawekezaji wa Kigeni Afrika
Katika makala yetu leo, Emmanuel Lubega anazungumzia msamaha wa kodi wanaopewa wawekezaji wa kigeni barani Afrika kwa muda fulani wakati wanapoanzisha shughuli zao. Hata hivyo suala hilo linapingwa vikali na wachumi barani Afrika.
Unalifahamu vipi tatizo la Usonji?
Ugonjwa wa Usonji au Autism ni tatizo la kibaiolojia ambalo kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, huathiri mtoto mmoja kati ya kila watoto 100 duniani. Dalili zake huanza kuonekana mapema sana, kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea. Ni vigumu kugundua dalili zake. Lakini kwenye video hii unaweza kujifunza mengi.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 2 wa 4
Ukurasa unaofuatia