You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Sauti zetu
Vidio zetu
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani
Matangazo
Wasichana wa Chibok
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Gavana wa Beki Kuu atimuliwa Nigeria
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria amemsimamisha kazi gavana wa Benki Kuu Sanusi Lamido ambaye amekuwa mkosaji mkubwa wa serikali kwa kutochukuwa hatua za kupambana na rushwa.
Dimba na CHAN laingia nusu fainali
Katika dimba la Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa timu za nyumbani, CHAN, Ghana, Libya, Nigeria na Zimbabwe zimeingia katika awamu ya nusu fainali mwishoni mwa wiki.
Nigeria, Mali zafuzu katika robo fainali ya CHAN
Nigeria iliziangamiza kabisa ndoto za wenyeji Afrika Kusini za kusonga mbele kutoka awamu ya makundi ya dimba la kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani - CHAN, baada ya kuwalaza magoli matatu kwa moja.
Maoni: Rais Jonathan 'ajikosha' kwa sheria dhidi ya ushoga
Wiki chache tu baada ya bunge kuupitisha mswaada wa kupiga marufuku ndoa za jinsia moja, Rais Goodluck Jonathan ameusaini kuwa sheria yumkini akitaka Wanigeria wamkumbuke angalau kwa hili ikiwa si kwa mengine yote.
Nchi tano zajiunga na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa
Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limezichagua nchi tano kuwa wanachama wapya wasiokuwa na viti vya kudumu wa baraza la usalama la umoja huo katika uchaguzi ambao haukuwa na ushindani mkali kama siku za nyuma
'Serikali Nigeria imeshindwa kuizuwia Boko Haram'
Makamo wa zamani wa rais wa Nigeria ameituhumu serikali ya nchi hiyo kwa kushindwa kushughulikia ugaidi kwa ufanisi, baada ya wapiganaji kuvamia bweni la wanafunzi na kuwaua 40 kati yao kaskazini mwa nchi hiyo.
Watu 44 wauwawa Nigeria
Watu wanaodhaniwa kuwa ni waislamu wenye itikadi kali wameshambulia kijiji na kuwauwa watu 44 huko kaskazini mashariki mwa Nigeria mapema wiki hii.(24.08.2013)
Boubakar Keita aongoza matokeo ya awali Mali
Keita anaongoza kwa idadi kubwa ya kura na huenda akashinda katika awamu ya kwanza ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili (28.07.2013). Nigeria imesema inaanza kuwandoa wanajeshi wake kutoka Mali hii leo.
Nigeria yashambuliwa kwa kumpokea al-Bashir
Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Nigeria wamefikisha kesi katika mahakama kuu mjini Abuja, wakiitaka kutoa waranti wa kumkamata rais wa Sudan Omar al-Bashir aliyekwenda huko kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika.
Nigeria kuumana na Tahiti
Mgogoro kuhusu marupurupu ambao ulitishia ushiriki wa Nigeria katika kinyang'anyiro cha FIFA cha kombe la mabara – FIFA Confederations Cup, kinachoendelea nchini Brazil ni kama haujatuliwa kikamilifu.
Goma, Nigeria na Afrika kusini magazetini
Mapigano Goma,kuzingirwa na jeshi,ngome ya wafuasi wa itikadi kali ya dini ya kiislam wa Nigeria- Maiduguri na mvutano kuhusu haki miliki ya jina la rais wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini Nelson Mandela magazetini
Hajiya Iyatu, Nigeria
Hajiya Iyatu ana umri wa miaka 58 na anaishi Bauchi, katikati ya Nigeria. Bibi huyo anatoa picha mchanganyiko kuhusu shughuli za Umoja wa Afrika.
Jeshi la Nigeria laendesha oparesheni kubwa dhidi ya wapiganaji wa Boko Haram
Mapigano makali yanaedelea nchini Nigeria kati ya Jeshi la Nigeria na wapaiganaji wa kundi la Boko Haram,ikiwa ni siku ya tano toka Jeshi la Nigeria kufanya operesheni ya kupambana na Boko haram mji wa Maiduguri
Jeshi la Nigeria laua wapiganaji wa Boko Haram
Ndege za kivita za Nigeria zimeshambulia kambi za wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo katika mapambano makubwa na kuzua onyo kali kutoka Marekani la kuheshimu haki za binadamu.
Afrika katika magazeti ya Ujerumani
Wiki hii magazeti ya Ujerumani yameandika juu ya mkutano wa kuchangisha fedha kwa ajili ya Mali, juu ya kodi kwa ajili ya maendeleo ya Afrika na pia yameandika juu ya ghasia zinazotokea nchini Nigeria
Jeshi la Nigeria lashambulia shabaha za Boko Haram
Vikosi vya serikali vimeanza kuzishambulia ngome za wapiganaji wa Kiislamu kaskazini-mashariki mwa Nigeria, katika operesheni ya kurudisha maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa kundi la Boko Haram.
Rais wa Nigeria atangaza hali ya hatari
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ametangaza hali ya hatari katika majimbo matatu nchini humo, na kuamrisha wanajeshi zaidi wapelekwe katika majimbo hayo ili kukabiliana na kundi la Kiislamu la Boko Haram.
Hali ya tete nchini Nigeria
Shirika la Umoja wa Mataifa la Haki za Binaadamu jana limeonesha kusikitishwa kwake na vurugu zinazoendelea huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria ambazo zimesababisha vifo na kuwaacha raia bila makazi
Watu 185 wauawa katika mapigano kati ya Boko Haram na jeshi la Nigeria
Watu 185 wameripotiwa kuuawa na wengine 2000 kuachwa bila makaazi, baada ya kutokea mapigano makali kati ya Jeshi na wanaoshukiwa kuwa waasi wa Kiislamu katika eneo la Baga, kaskazini-mashariki mwa Nigeria.
Ustawi haujapunguza umasikini Afrika
Nchi za Afrika zinastawi katika viwango vya uchumi vya kuonewa gele na nchi za viwannda. Lakini unomi huo umeshindwa katika miaka ya karibuni kuvipunguza viwango vya umasikini miongoni mwa watu
Mataifa ya EU yaonywa
Umoja wa Ulaya umezionya nchi wanachama wa Umoja huo kuweka mikakati imara dhidi ya biashara ya kuuza binaadamu isiokubalika au ziwekewe vikwazo.
Mafuta ya Nigeria
Nigeria ina hazina kubwa ya mafuta. Lakini haijaweza kuwaletea wakaazi wake hali bora ya maisha.
Raia 7 wa kigeni wauwawa Nigeria
Italia na Ugiriki zimethibitisha kuwa raia saba wa kigeni waliotekwa nyara kutoka kampuni moja ya ujenzi mwezi uliopita na kundi haramu la Ansaru nchini Nigeria wameuwawa.
Afrika katika magazeti ya Ujerumani
Wiki hii magazeti ya Ujerumani yameandika juu ya mwanaharakati Mamphela Ramphele anaekusudia kukipa changamoto chama cha ANC, nchini Afrika Kusini na juhudi za kupambana na njaa barani Afrika.
Opereshini za kijeshi zaingia awamu ya mwisho Mali
Jeshi la Ufaransa na lile la Mali,limeanzisha hujuma katika milima ya Ifoghans kaskazini.Wanajeshi 2 wa Ufaransa wameuwawa.Raia wa Ufaransa wametakiwa waondoke kaskazini ya Camerun.
Afrika katika magazeti ya Ujerumani
Pamoja na mengine wiki hii magazeti ya Ujerumani yameandika habari za kushtusha juu ya mwanamichezo maarufu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius.
AFCON 2013; Nigeria kutoroka na kombe?
Nigeria inaonekana karatasini inaweza kutoroka na taji la ubingwa wa kombe la mataifa ya Afrika leo jioni(10.02.2013)ikipata ushindi wake wa tatu katika mashindano haya katika uwanja wa soccer City mjini Johannesburg.
Mali na Ghana historia itajirudia?
Mali ina matarajio kuwa historia itajirudia yenyewe Jumamosi(09.02.2013)wakati itakapokutana na Ghana,kwa ajili ya mchezo wa kuwania medali ya shaba katika kombe la Afrika,AFCON 2013, nchini Afrika kusini.
Nigeria, Burkina Faso nani zaidi Fainali?
Nigeria na Burkina Faso zitakutana katika fainali ya mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika katika uwanja wa Soccer City siku ya Jumapili, baada ya timu zote kupata ushindi mkubwa katika hatua ya nusu fainali Jumatano.
Ndoto ya Cote D'Ivoire yaota mbawa
Nigeria na Burkina Faso zakamilisha orodha ya timu nne zilizoingia katika nusu fainali ya kombe la mataifa ya Afrika huko Afrika kusini.Borussia Dortmund yanyakua nafasi ya pili ligi ya Ujerumani Bundesliga.
Zambia yapigwa kumbo AFCON 2013
Timu ya kandanda ya taifa ya Zambia, Chipolopolo, imekuwa mabingwa watetezi wa kwanza kupigwa kumbo kwenye michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika kwenye mechi za makundi katika kipindi cha miaka 21 iliyopita.
Wanajeshi 1,000 wa Afrika wawasili Mali
Huku vikosi vya Ufaransa vikizidi kusonga mbele katika juhudi za kuwaondoa waasi kaskazini mwa Mali, wanajeshi wengine 1,000 wa Kiafrika wamewasili nchini humo kusaidia kuwaondoa kabisa waasi kaskazini mwa nchi hiyo.
Vidio: Mafuta ya Nigeria
Petroli husafishwa kwa wingi Nigeria - katika mazingira magumu.
Usafishaji wa mafuta usio halali
Petroli husafishwa kwa wingi Nigeria - katika mazingira magumu.
Jeshi la Afrika kuwekwa Mali
Kikundi cha kwanza cha wanajeshi 900 wa Nigeria kwenda nchini Mali kitafika huko katika saa 24 zijazo kama sehemu ya jeshi la Afrika lililopewa uwezo huo na umoja wa mataifa.
Kampeni ya ndoa za jumla-jamala na mafanikio yake Nigeria
Nchini Nigeria, kunaendeshwa kampeni maalum ya kuwafungisha ndoa wanaume na wanawake wanaohitaji kuingia kwenye taasisi hiyo ya kijamii wakiwa na sababu na mahitaji tafauti, katika mtindo wa ndoa za kupanga.
ICC yaanza kuichunguza Boko Haram
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Fatou Bensouda, ameitaka serikali ya Nigeria kuchunguza uhalifu unaofanywa na kundi la Boko Haram baada ya Mahakama yake kuanza kulifuatilia kundi hilo.
Waziri wa Ulinzi na mshauri wake watimuliwa Nigeria
Rais Goodluck Jonatahan wa Nigeria, amemfukuza kazi Waziri wa ulinzi pamoja na mshauri wake, hku kukiwana ongezeko jipya la mashambulizi kutoka kwa kundi la wanamgambo wa kiislamu wenye msimamo mkali la Boko Haramu.
Viongozi Boko Haram waingizwa orodha ya magaidi
Marekani kwa mara ya kwanza imewaweka viongozi watatu wanatuhumiwa kuongoza kundi la Boko Haram lililopo eneo la Maiduguri, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, katika orodha ya magaidi wa Kimataifa.
Afrika Katika Magazeti ya Ujerumai ,Boko Haram waendelea kuua watu
Wiki hii magazeti Ujerumani yameandika juu ya matukio ya kaskazini mwa Afrika,ambako jeshi la Misri linajaribu kuzuia juhudi za kuleta demokrasia. Pia yameandika juu ya Nigeria.
Juhudi za kupambana na ugaidi nchini Nigeria
Jinsi mji wa kaskazini wa Nigeria Kano unavyojitahidi kurejesha hali ya kuaminiana miongoni mmwa jamii na waislam na wakristo,licha ya vitisho vya kigaidi vya Boko Haram
Nigeria inapata hasara kwa wizi wa mafuta
NIgeria: Wizi wa mafuta yasiyosafishwa ni tatizo linalolikosesha taifa hilo mapato mengi.
Nigeria kuimarisha usalama wa safari za ndege
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan hii leo (04.06.2012) ameahidi kuchukua hatua madhubuti kuimarisha usalama wa usafiri wa ndege nchini humo kufuatia ajali ya ndege hapo jana ambapo zaidi ya watu 150 waliuwawa.
Ujerumani na Nigeria kuongeza ushirikiano
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria leo anamaliza ziara yake ya siku tatu Ujerumani. Miongoni mwa masuala aliyoyajadili na wenyeji wake ni mahusiano ya kibiashara pamoja na vita dhidi ya kundi la Boko Haram.
Magazeti ya Ujerumani yaandika juu ya Mali,Boko Haram na hatari ya mitumba
Magazeti ya Ujerumani wiki hii yameandika juu ya mgogoro wa Mali, Mkataba wa amani baina ya Sudan na Sudan ya kusini na juu ya kundi la wanaitikadi kali wa kiislamu Boko Haram la nchini Nigeria.
Wimbi la mashambulio laendelea Nigeria
Miripuko mipya imeutikisa mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeria asubuhi ya leo. Miripuko hiyo na milio ya risasi ilisikika katika mji huo wa kaskazini,ambako Ijumaa hadi watu 185 waliuawa katika msururo wa mashambulio.
Rais Jonathan aapa kuwaadhibu wafadhili wa Boko Haram
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria amesema watu wanaoshukiwa kuhusika na mashambulizi ya wiki iliyopita mjini Kano, ambayo yameua zaidi ya watu 160 wameanza kukamatwa huku akiapa tena kuliangamiza kundi la Boko Haram.
Waliokufa kwenye miripuko ya Nigeria wafikia 160
Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na mashambulizi ya mabomu yaliyofanyika katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Nigeria, Kano, Ijumaa iliyopita (20.01.2012) nchini Nigeria imepanda na kufikia 160.
Idadi kubwa ya watu wauwawa Nigeria
Takribani miili ya watu 120 imerundikana katika chumba cha kuhifadhia maiti huko katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Nigeria, Kano baada ya kutokea kwa mashambulio ya mabomu na risasi usiku uliyopita.
21.01.2012
Majeshi ya usalama ya Nigeria yameweka amri ya kutotembea katika mji wa Kano, baada ya shambulio la bomu na kusababisha watu wanane kuuwawa.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 15 wa 19
Ukurasa unaofuatia