1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi kubwa ya watu wauwawa Nigeria

21 Januari 2012

Takribani miili ya watu 120 imerundikana katika chumba cha kuhifadhia maiti huko katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Nigeria, Kano baada ya kutokea kwa mashambulio ya mabomu na risasi usiku uliyopita.

https://p.dw.com/p/13niZ
Smoke rises from the police headquarters as people run for safety in Nigeria's northern city of Kano January 20, 2012. At least six people were killed in a string of bomb blasts on Friday in Nigeria's second city Kano and the authorities imposed a curfew across the city, which has been plagued by an insurgency led by the Islamist sect Boko Haram. There was no immediate claim of responsibility for the apparently coordinated attacks. REUTERS/Stringer (NIGERIA - Tags: CRIME LAW CIVIL UNREST TPX IMAGES OF THE DAY)IL UNREST)
Milipuko mjini KanoPicha: Reuters

Mwandishi wa Shirika la Habari la Ufaransa AFP aliyehesabu miili ya watu hao katika hospitali kuu mjini Kano, amesema mingi imeonekana kuwa na majeraha ya risasi. Kiasi ya watu 100 wamekuwa wakisubiri nje ya chumba cha maiti kuchukua miili ya jamaa zao. Akielezea hali ilivyokuwa shuhuda mmoja alisema "Kumesikika sauti ya milipiko kama minne. Na kuna miiili ya watu watatu mbele ya ofisi ya uhamiaji. Na pia tulisikia milipuko kadhaa ya mabomu na risasi mbele ya kituo cha polisi". alisema shuhuda huyo. Kundi la Waislam wenye msimamo mkali la Boko Haram limekiri kuhusika na mauwaji hayo.