1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wimbi la mashambulio laendelea Nigeria

Martin,Prema/afpe24 Januari 2012

Miripuko mipya imeutikisa mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeria asubuhi ya leo. Miripuko hiyo na milio ya risasi ilisikika katika mji huo wa kaskazini,ambako Ijumaa hadi watu 185 waliuawa katika msururo wa mashambulio.

https://p.dw.com/p/13os4
and the authorities imposed a curfew across the city, which has been plagued by an insurgency led by the Islamist sect Boko Haram. There was no immediate claim of responsibility for the apparently coordinated attacks. REUTERS/Stringer (NIGERIA - Tags: CRIME LAW CIVIL UNREST)
Miripuko mipya yautikisa mji wa KanoPicha: Reuters

Mapigano ya asubuhi ya leo, yalizuka baada ya kiasi ya miripuko 15 kutokea katika eneo lililo karibu na kituo cha polisi. Milio ya risasi iliendelea kusikika hata baada ya miripuko hiyo kusita. Mashahidi wamesema, hadi watu 2 wameuawa asubuhi ya leo, baada ya vikosi vya usalama kuizingira nyumba iliyoshukiwa kutumiwa kama maficho ya wanamgambo wa kundi la Kiislamu la Boko Haram.

Hapo jana, polisi walifanikiwa kuzuia mashambulio, baada ya kugundua magari 10 yaliyotegwa mabomu na miripuko mingine, katika mji wa Kano ulio wa pili kwa ukubwa nchini Nigeria. Mkuu wa polisi Ibrahim Idris amesema, raia 150, polisi 29 na maafisa wengine 6 wameuawa katika mashambulio ya Ijumaa katika mji huo wa Kano ulio na wakaazi milioni 4.2 wengi wao wakiwa ni Waislamu.

©Jonathan Rebboah/Wostok Press/Maxppp France, Paris 25/11/2011 Le president du Nigeria Goodluck Jonathan arrive au palais de l Elysee The President of Nigeria Goodluck Jonathan at the Elysee Palace
Rais Goodluck Jonathan ameahidi kuimarisha usalamaPicha: picture alliance / dpa

Rais wa nchi hiyo, Goodluck Jonathan ameahidi kuimarisha usalama huku akipambana na mzozo mbaya kabisa tangu kushika madaraka miezi tisa iliyopita, wakati wimbi la machafuko likizidi nchini humo na kundi la Boko Haram likilaumiwa kwa ghasia hizo. Desemba 31, Jonathan alitangaza hali ya hatari katika baadhi ya maeneo ya kaskazini, kufuatia wimbi la mashambulio. Kundi la Boko Haram limetuhumiwa kuhusika na mashambulio hayo vile vile.

Mshindi wa zawadi ya uandishi sanifu ya Nobel, Wole Soyinka aliewahi kuonya juu ya hatari ya kuibuka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo, sasa ametoa mwito kwa Wanigeria wenzake, kutolipizana kisasi. Hata viongozi wa kisiasa wanajaribu kuhakikisha kuwa machafuko ya hivi sasa, hayatochochea mzozo mkubwa zaidi, katika nchi hiyo ambako Waislamu wengi huishi kaskazini mwa nchi wakati eneo la kusini likiwa na Wakristo zaidi.

Nigerian Wole Soyinka, Literature Nobel Laureate in 1985, delivers her speech during the 2nd edition of the Geneva Lectre Series on the theme "Are human rights universal?", on the occasion of the 60th anniversary of the Universal Declaration of Human Rights at the European headquarters of the United Nations in Geneva, Switzerland, Wednesday, Dec. 10, 2008. (AP Photo/Keystone, Salvatore Di Nolfi)
Wole Soynika, mshindi wa zawadi ya uandishi sanifu ya NobelPicha: AP

Wakati huo huo, mtu aliedai kuwa msemaji wa Boko Haram, amesema, wamefanya mashambulio hayo kwa sababu serikali, imekataa kuwaachilia wanachama wenzao walio kizuizini. Inaaminiwa kuwa baadhi ya wafungwa hao walitoroka, baada ya kituo cha polisi kushambuliwa Ijumaa iliyopita.