1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Japan kuendeleza marekebisho ya katiba

Hawa Bihoga
11 Julai 2022

Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida ameahidi kufanyia kazi mabadiliko ya katiba na sera nyingine muhimu yaliyoanzishwa na mtangulizi wake Shinzo Abe aliyeuawa kwa kupigwa risasi Jumaa iliyopita kwenye mkutano wa siasa.

https://p.dw.com/p/4DxBe
Japan Oberhauswahlen | Premierminister Fumio Kishida und Liberaldemokratische Partei
Picha: The Yomiuri Shimbun/AP Images/picture alliance

Kishida amesema hayo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari leo Jumatatu baada ya chama chake kupata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa wabunge uliofanyika Jana Jumapili.

Amesema viti ambavyo chama chake chaLDP kimeshinda haviwakilishi tu mamalaka ambayo wajapan wametoa kwa muungano unaotawala, bali amechukulia kama matakwa ya wananchi kuchochea umoja huo kufanya kazi kwa uwezo wake wote katika kuilinda Japan na kufungua mustakabali wa baadae.

Ameongeza kwamba kwa upande wake ana mtazamo mpya katika dhana ya uwajibikaji, ikiwa ni pamoja na kuangalia yote ambayo Abe alitamani kuyafanya kwa Japani.

Soma zaidi:Shinzo Abe afariki dunia baada ya kupigwa risasi

Akizungumzia kifo cha Abe ikiwa ni siku tatu tu tangu alipopigwa risasi  akiwa katika jukwaa la kisiasa, Kishida ameahidi kufuata nyayo za waziri mkuu huyo wa zamani.

Amewaambia wanahabari kwamba atakabiliana na changamoto kadha wa kadhaa ikiwemokuifanyia marekebisho katiba, kadhalika kutekwa kwa raia  na mawakala wa Korea Kaskazini.

"Tutarithi matamanio ya waziri mkuu wa zamani Abe na kukabiliana na masuala magumu" Alisema katika mkutano wake na waandishi wa hababri punde baada ya chama chake kushinda katika uchaguzi hapo jana.

Aliongeza kwamba mambo hayo kwa serikali yake ni muhimu katika kuyatimiza kwani waziri wa zamani Abe ambae pia ni alikuwa mwanansiasa mwenye ushawishi mkubwa hakuweza kuyatimiza."

Kishida:Japani inahitaji siasa zitachoshughulikia dharura za nchi

Kishida amesema kwa sasa Japan inapitia kipindi kigumu tangu baada ya vita na kwamba kinachohitajika kwa sasa ni siasa ambazo zitaweza kushughulikia hali ya dharura.

Japan Tokio | Parlament
Bunge la Japani likiwa katika shughuli zake za kawaidaPicha: Masanori Genko/AP Photo/picture alliance

Kambi ya wafuasi wanaotaka mabadiliko ya katiba - mbali ya vyama vyamuungano - pia vyama viwili vya upinzani vya kihafidhina imepata theluthi mbili zinazophitajika katika uchaguzi huo wa bunge.

Abe aliamini kwamba katiba iliopo haikuwa inaendana na matakwa ya sasa ya Japani kama taifa huru kwa sababu ilitengenezwa mwaka 1945 na Marekani iliyokuwa inaikalia wakati huo.

Soma zaidi:Viongozi waomboleza kifo cha waziri Mkuu mstaafu Shinzo Abe

Kwa hivi sasa Marekani imekuwa ni mshirika wa karibu wa Japani katika masuala ya uliinzi.

Leo Jumatatu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ametoa salamu za rambirambi kwa serikali ya waziri mkuu Kishida kwa kifo cha aliekuwa waziri mkuu wa zamani Abe, Blinken akiwa njiani kutoka nchini Thailand alibadili ratiba ya ziara yake na kuwasili mjini Tokyo kwa ajili ya maombolezo.