1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump aapa kuendelea na kiny'ang'anyiro cha urais

29 Julai 2023

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema hatasitisha kinyang'anyiro chake cha kugombea urais iwapo atakutwa na hatia na kuhukumiwa katika uchunguzi wowote wa uhalifu unaotishia kukwamisha azma yake.

https://p.dw.com/p/4UX6C
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald TrumpPicha: Gerald Herbert/AP Photo/picture alliance

Alipoulizwa na mtangazaji wa redio John Fredericks ikiwa kuhukumiwa kwake kutasimamisha kampeni yake, Trump alijibu hapana na kwamba hakuna chochote katika Katiba kinachomzuia kugombea ikiwa atakutwa na hatia.

Mgombea huyo wa chama cha Republican alikuwa akijadili mashtaka mengi yanayomkabili wakati anapojiandaa kugombea muhula wa pili wa urais, siku moja baada ya waendesha mashtaka kuongeza mashtaka dhidi yake kuhusu namna alivyoshughulikia nyaraka za siri za serikali.

Spma zaidi: Trump akabiliwa na mashtaka mapya katika kesi ya nyaraka zenye siri nzito za serikali

Rais huyo wa zamani ambaye ameshtakiwa mara mbili, alishtakiwa kwa mara ya kwanza mwezi uliopita akituhumiwa kuhatarisha usalama wa taifa kwa kuhodhi taarifa za siri kuhusu nyuklia na ulinzi, baada ya kuondoka katika Ikulu ya Marekani.