1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump akana makosa katika kesi ya kuhodhi nyaraka za siri

14 Juni 2023

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amekana mashtaka, akiwa anakabiliwa na makosa kadhaa ya ufujaji wa nyaraka za siri za serikali.

https://p.dw.com/p/4SXp6
USA Prozess gegen Ex-Präsident Trump in Miami
Picha: Alon Skuy/Getty Images

Hatua hiyo inamaanisha kwamba inaweza kuchukua mwaka mmoja au zaidi hadi kesi kuanza kusikilizwa.

Kesi hiyo ya kiserikali inasema Trump alihifadhi hati za usalama wa kitaifa kinyume cha sheria alipoondoka madarakani na kuwadanganya maafisa ambao walitaka kuzirejesha.

Inadaiwa rais huyo wa zamani wa Marekani anatuhumiwa kuhodhi nyaraka za siri za serikali, kuwaonyesha wageni na kujaribu kuzificha dhidi ya timu ya wachunguzi.

Soma pia: Trump akana mashtaka ya nyaraka za siri

Kimsingi Trump anakabiliwa na tuhuma za makosa 37 ambayo yanamuhisishwa kwa kuhifadhi kwa makusudi nayaraka za siri ambazo waendesha mashtaka wanasema zingeweza kuhatarisha usalama wa taifa iwapo zitafichuliwa. Kesi hiyo inaweza kuwa na matokea makubwa kisheria kwa kuwa na uwezekano wa hukumu ya miaka mingi gerezani.