1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump asema hataacha kuwania urais

28 Julai 2023

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump amesema leo kuwa hatositisha kampeni yake ya kuwania urais mwaka 2024 hata iwapo atakutwa na hatia.

https://p.dw.com/p/4UWIe
US-Wahlen 2024 | Trump
Picha: Charlie Neibergall/AP Photo/picture alliance

Donald Trump ameyasema hayo katika mahojiano kwenye kipindi cha redio cha John Fredericks, siku moja tu baada ya kukabiliwa na mashtaka mapya ya kumiliki nyaraka zilizoanishwa kuwa "siri ya serikali."

Awali, waendesha mashtaka nchini humo walidai kuwa Trump alimtaka mfanyakazi wake kufuta picha za kamera katika makaazi yake mjini Florida katika juhudi za kuzuia uchunguzi juu ya nyaraka hizo.

Mashtaka mapya yanajumuisha kuzizuia kwa makusudi taarifa nyeti za ulinzi wa taifa, na kuongeza maelezo mapya katika kesi ya jinai iliyofunguliwa dhidi ya rais huyo wa zamani na msaidizi wake wa karibu.