1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Kesi ya Trump itaanza kusikilizwa Mei 2024

21 Julai 2023

Jaji wa Mahakama ya wilaya nchini Marekani anaesimamia kesi ya kutumia vibaya nyaraka za siri dhidi ya rais wa zamani, Donald Trump, Aileen Cannon amesema wataanza kusikiliza kesi hiyo Mei 24, mwakani.

https://p.dw.com/p/4UEod
USA | Donald Trump
Picha: John Angelillo/UPI Photo/IMAGO

Trump atakuwa rais wa kwanza wa zamani kushtakiwa kwa uhalifu. Waendesha mashtaka walikuwa wameomba kesi hiyo ianze Desemba mwaka huu, huku mawakili wa utetezi wa Trump wakiomba ianze baada ya uchaguzi wa rais wa Novemba 2024.

Soma pia: Trump akana makosa katika kesi ya kuhodhi nyaraka za siri

Trump mwenye umri wa miaka 77 ndiye mgombea anaepewa nafasi kubwa kuteuliwa na wanachama wa Republican kugombea dhidi ya rais Joe Biden katika uchaguzi ujao, na kesi hiyo itasikilizwa katika kiele cha kampeni za mchujo cha kumteua mgombea urais wa chama hicho kikongwe, kinachofahamika kama GOP.