1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel: Yawaamuru wanajeshi kulizingira Ukanda wa Gaza

9 Oktoba 2023

Serikali ya Israel leo imewaamuru wanajeshi wake kulizingira kabisa eneo la Ukanda wa Gaza hatua ambayo imesimamisha uingiaji wa chakula, mafuta na mahitaji mengine kwenye eneo hilo lenye watu wapatao milioni 2.3.

https://p.dw.com/p/4XJYw
Moshi ukifuka hewani baada ya mashambulizi ya israel katika ukanda wa Gaza
Moshi ukifuka hewani baada ya mashambulizi ya israel katika ukanda wa GazaPicha: Mahmud Hams/AFP

Wakati huo huo, wanajeshi wa Israel wamefanya mashambulizi ya anga kwenye eneo linalotawaliwa na kundi la Hamas katika hatua ya kulipiza kisasi mashambulio ya wanamgambo hao ya mwishoni mwa wiki.

Zaidi ya siku mbili baada ya Hamas kuanzisha mashambulizi ya kushtukiza kutokea Ukanda wa Gaza, jeshi la Israel limesema kwakiasi kikubwa limerudisha udhibiti katika miji ya kusini ambako limekuwa likipambana na wapiganaji wa Hamas.

Soma pia:Miito ya mataifa imeanzia kuiunga mkono Israel na kulaani vikali mashambulizi ya Palestina, huku wengine wakiipongeza Hamas

Wakati huo huoc, Tume ya Umoja wa Ulaya imesema inapitia upya misaada yake ya maendeleo kwa Wapalestina, yenye thamani ya euro milioni 691 na kwamba imesimaisha malipo mara moja.