1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kaskazini yafanya majaribio mengine ya makombora

22 Julai 2023

Korea Kaskazini imefyetua "makombora kadhaa ya masafa marefu" usiku wa kuamkia leo kuelekea Bahari ya Njano inayopatikana kati ya China na Rasi ya Korea.

https://p.dw.com/p/4UFn6
Televisheni za Korea Kusini zikionesha makombora yaliyorushwa na Korea Kaskazini
Televisheni za Korea Kusini zikionesha makombora yaliyorushwa na Korea KaskaziniPicha: Ahn Young-joon/AP Photo/picture alliance

Hayo yameripotiwa na shirika la habari la Korea Kusini, Yonhap likinukuu maafisa wa jeshi la nchi hiyo. Ufyetuaji huo umefanyika ikiwa zimepita siku tatu pekee tangu nchi hiyo ilipofanya majaribio mengine ya makombora mawili ya masafa  marefu wakati mivutano inaongezeka kwenye eneo la rasi ya korea.

Soma zaidi: Marekani, Japan na Korea Kusini zalaani hatua ya Korea Kaskazini kurusha kombora

Wakati hayo yakijiri kundi la mataifa tajiri la G7 na nchi nyingine tatu zimeandika barua kwenda kwa China ya kuitaka nchi hiyo isaidie kuizuia Korea Kaskazini kuepuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa kwa kutumia eneo la bahari la China.

Kundi hilo la mataifa ya G7 na washirika wengine limesema lina mashaka juu ya uwepo kwa meli za mafuta kwenye eneo la bahari la China la Sansha Bay ambazo inaamini zinafanya biashara ya mafuta na Korea Kaskazinina kukwepa vikwazo ilivyoewekewa nchi hiyo na Umoja wa Mataifa.