1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Japan itaharibu kombora litakalorushwa na Korea Kaskazini

29 Mei 2023

Japan imesema itakayaharibu makombora ya Korea Kaskazini yatakayoelekezwa nchini mwake, na kusisitiza inajiandaa kufanya hivyo.

https://p.dw.com/p/4RvvZ
Erneuter Raketentest in Nordkorea im November 2022
Picha: KCNA/KNS/STR/AFP

Korea Kaskazini imesema imekamilisha satelaiti yake ya kwanza ya kijeshi ya ujasusi na tayari kiongozi wake Kim Jong Un ameidhinisha maandalizi ya mwisho ya kuipeleka angani.

Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida tayari ameziagiza mamlaka husika kukusanya na kuchambua taarifa za kijasusi na kuongeza hatua kama hizo zinakiuka sheria za kimataifa.

"Matumizi ya teknolojia ya makombora ya nyuklia yatakiuka maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na yanaweza kuibua kitisho kikubwa na wasiwasi wa usalama kwa watu wa Japan.", alisema Kishida.

Kishida aidha amesema anashirikiana kwa karibu na Marekani na Korea Kusini, huku akiiomba Pyongyang kuachana na hatua hiyo.

Wachambuzi wanasema satelaiti ya kijeshi inaweza ikaimarisha uwezo wa Korea Kaskazini wa kijasusi na kushambulia maeneo inayoyalenga kunapotokea vita.