1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yasema imefanya majaribio ya makombora

24 Februari 2023

Korea Kaskazini imesema imefanya majaribio ya makombora ya masafa marefu katika pwani yake ya mashariki siku moja kabla ya kuongeza mfululizo wa matumizi ya silaha wakati wapinzani wake wakiongeza mafunzo ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4NvW7
Nordkorea Raketentest
Picha: Ahn Young-joon/AP Photo/picture alliance

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimesema urushaji huo wa makombora ambao uliothibitishwa na jeshi la Korea Kusini, ulikusudiwa kuthibitishwa kutegemewa kwa makombora hayo na uwezo wa kujibu kwa haraka kitengo kinachoongoza silaha hizo.

Shirika la habari la Pyongyang limeripoti kwamba makombora hayo manne yaliruka kwa karibu saa tatu baada ya kurushwa kutoka pwani ya kaskazini mashariki, yalionesha yanaweza kulenga shabaha kilometa 2,000.

Hata hivyo taarifa ya pamoja kati ya Korea Kusini na mshirika wake Marekani zimekosoa juu ya taarifa hiyo bila kufafanua zaidi.