1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Makombora ya Korea kaskazini yanakiuka maazimio ya UN

15 Julai 2023

Marekani, Korea Kusini na Japan zimelaani hatua ya Korea Kaskazini kurusha kombora la masafa marefu wiki hii na kusema nchi hiyo inakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa na kutishia amani katika kanda ya Asia ya Mashariki.

https://p.dw.com/p/4TwR2
Moja ya majaribio ya kurusha makombora ya Korea kaskazini
Moja ya majaribio ya kurusha makombora ya Korea kaskaziniPicha: KCNA via REUTERS

Katika taarifa ya pamoja, wanadiplomasia wakuu wa Marekani, Korea Kusini na Japan wameeleza kuwa urushaji wa kombora hilo kunatishia amani sio tu katika rasi ya Korea bali katika sehemu nyingine za dunia.

Nchi hizo tatu zimeihimiza Korea Kaskazini kukomesha kile walichokiita "uvunjaji wa sheria na kuchochea mzozo wa kidiplomasia, na badala yake inafaa kurudi kwenye mazungumzo."

Soma zaidi: Korea Kaskazini yafanya jaribio la kombora la masafa marefu

Kombora hilo, lililorushwa kwenye pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini, liliruka kwa muda wa dakika 7 na kwa umbali wa kilomita 1,000 katika kile kinachoelezwa kuwa muda mrefu zaidi wa kombora la Korea Kaskazini kukaa angani.