1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky asifia mifumo ya ulinzi ya Marekani, Ujerumani

7 Agosti 2023

Rais Volodymyr Zelenskiy amesema nchi yake inayashuhudia matokeo chanya ya mifumo ya ulinzi wa anga kutoka Marekani na Ujerumani licha ya msururu wa mashambulizi ya Urusi yaliyolenga makaazi ya raia mjini Kyiv.

https://p.dw.com/p/4UqZQ
Ukraine Kiew | Videoansprache Wolodymyr Selenskyj
Picha: president.gov.ua

Zelenskiy amesema mifumo ya IRIS-T na Patriot imesaidia kuzuia sehemu kubwa ya mashambulizi ya Urusi wiki iliyopita ikiwa ni pamoja na kudunguwa makombora 65 na ndege zisizo na rubani zipatazo 178 za Urusi.

Soma zaidi: Shambulizi la Urusi laua mtu mmoja, 23 wamejeruhiwa Mykolaiv

Urusi imesema imedungua ndege isiyo na rubani iliyokuwa ikielekea Moscow katika shambulio la tatu kama hilo ndani ya wiki moja, wakati maafisa wa pande zote mbili wakisema Ukraine iliyashambulia madaraja mawili yanayounganisha Crimea na Urusi.

Urusi na Ukraine zimekuwa zikishambuliana na kulenga miundombinu ya kimkakati ya adui ikiwa ni pamoja na maghala ya silaha, madaraja na meli za kivita.