1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wiki ya kumbukumbu ya mauwaji ya kimbari nchini Rwanda

7 Aprili 2022

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameyalaumu mataifa makubwa ambayo hakuyataja majina kwa kukaa kimya wakati nchi yake ilipokuwa ikipitia jinamizi la mauaji ya kimbari miaka 28 iliyopita.

https://p.dw.com/p/49c83
Gedenken an den Genozid in Ruanda
Picha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Siku ya tarehe 7 ya mwezi wa nne kila mwaka ni mwanzo wa juma la kuwakumbuka watu wapatao milioni moja waliouawa katika mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994. Kuanzia asubuhi wananchi kuanzia ngazi ya kijiji walikusanyika pamoja ambapo walisikiliza historia ya jinsi mauaji hayo yalivyotokea, sababu yake na namna taiafa lilivyojikwamua hadi hapa lilipo

Lakini katika mihadhara iliyotolewa leo kote nchini baadhi ya wananchi wameonyesha wasiwasi kwamba wakati Rwanda ikikumbuka mauaji haya kwa upande mwingine mitandao ya kijamii kutoka ndani na nje ya Rwanda inaingia kwenye mrengo uleule wa vyombo vya habari vilivyoeneza ya mauaji hayo.

''Kwa sasa tumechukua uamuzi wa kuanza kuwajibu kwa sababu makala zao zinatisha ila sisi tuliopo hapa tumeamua kila tukiona makala za hivi tunawajibu kwa kuwaeleza kuwa wanachokisema si kweli hapa.Kwa kufanya hivi tunaamini na wao pengine watajua ukweli...''

Soma pia→Human Rights Watch yalaani ukandamizaji nchini Rwanda

''Wanafanya hivi kwa kupuuza kile kilichotokea''

Ruanda Symbolbild Völkermord
Picha: picture-alliance/AP Photo/R. Mazalan

'' Tunajaribu kuwaeleza kuwa kwa kufanya kumbukumbu kama za leo tunataka tusije kujikuta tunarejea huko kwa sababu sisi ni binadamu tuna kasumba ya kusahau...na wao wanafanya hivi kwa kupuuza kile kilichotokea.'''

Akizungumza katika maadhimisho haya Rais wa Rwanda Paul Kagame amezilaumu nchi kubwa ambazo hata hivyo hakuzitaja majina akihoji kwamba zinapata wapi ujasiri wa kutoa mafunzo kwa Rwanda wakati nchi hizo hizo zilikuwa na mkono kwenye mauaji hayo

''Sisi ni nchi ndogo lakini ni wakumbwa mno kwenye haki na baadhi ya hao mnaowasikia ni nchi kubwa na zenye nguvu lakini ni wadogo sana katika suala la haki..hawana mamlaka ya kutoa mafunzo kwa mtu yeyote...kwa sababu wao ni sehemuya historia hii ambapo zaidi ya watu wetu milioni wakiangamizwa.''

Soma pia→Rwanda yadai mkoasoaji wake aliyetoweka aliingia Uganda

Rwanda yapiga hatua ya maendeleo ?

Paul Kagame
Picha: Picture alliance/AP Photo/E. Murinzi

Rais Paul Kagame amesema wananchi sasa wameweza kupiga hatua ya maendeleo kutokana na sera inayoendelea kufanikiwa ya umoja na maridhiano ambayo kimsingi haikuwa rahisi kufikiwa.

''Hebu wewe fikiria baadhi yetu sisi tuliokuwa na silaha, kama tungejiruhusu kuwaendea wale waliokuwa wakifanya mauaji ya watu wetu na kuwaua kiholela kama ambavyo walikuwa wakiwaua ndugu zetu...kwanza tungelikuwa na haki ya kufanya hivyo...lakini hatukuchukua hatua hiyo tuliwaacha...''

Kwa mara ya kwanza miaka miwili iliyopita wananchi sasa kuanzia asubuhi waliweza kukutana pamoja na kupeana ushuhuda wa kile kilichotokea miaka 28 iliyopita. Miaka miwili iliyopita hili haliwezekana kutoka na janga la corona.