1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Watunisia wajitokeza kwa uchache kupiga kura

Hawa Bihoga
24 Desemba 2023

Wapiga kura nchini Tunisia wameitikia zoezi la kupiga kura leo Jumapili katika uchaguzi wa wawakilishi wa baraza la pili la Bunge chini ya katiba iliyoungwa mkono mwaka jana na Rais Kais Saied.

https://p.dw.com/p/4aXjf
Tunesien Parlamentswahlen Wahllokal
Picha: Hasan Mrad/Zuma/picture alliance

Kulingana na Mamlaka Huru ya Uchaguzi nchini humo ISIE, wapiga kura wa Tunisia watachagua wawakilishi 2,000 kati ya wagombea 7,000 waliojitokeza kuomba ridhaa ya wananchi kuwawakilisha.

Uchaguzi huo utawezesha kuanzishwa kwa mabaraza ya mitaa, mikoa na wilaya na kuruhusu kuundwa kwa Bunge la pili.

Wapinzani wa Rais Saied wametoa wito wa kususia uchaguzi wa leo Jumapili na kuutaja kuwa sio halali.

Zaidi ya watu mashuhuri 260 nchini Tunisia walitia saini ombi la kupinga kile walichokiita "uchaguzi usiokuwa na maana," wakiamini kuwa serikali ya Saied inaendelea kutekeleza miradi yake ya kisiasa.

Tangu mapema mwaka huu mamlaka imewafunga jela zaidi ya wanachama 20 wa upinzani, akiwemo kiongozi wa Ennahdha Rached Ghannouchi na Jawhar Ben Mbarek, mwanzilishi mwenza wa chama cha National Salvation Front, miongoni mwa wengine.