1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tunisia yawazuia karibu wakimbizi 2,500 kwenda Ulaya

20 Septemba 2023

Walinzi wa Tunisia wamefanikiwa kuwazuia wahamiaji 2,507 waliokuwa wakijaribu kwenda Ulaya kupitia Bahari ya Mediterania na kuwakamata watu 62 wanaosafirisha watu kwa njia za haramu.

https://p.dw.com/p/4Wax7
Tunisia imesema imeanzisha operesheni kubwa ya kusimamisha biashara haramu ya binaadamu na kuzuia idadi kubwa ya watu wanaokufa katika safari za mateso za baharini
Tunisia imesema imeanzisha operesheni kubwa ya kusimamisha biashara haramu ya binaadamu na kuzuia idadi kubwa ya watu wanaokufa katika safari za mateso za bahariniPicha: Hasan Mrad/ZUMA/IMAGO

Msemaji wa Kikosi cha kitaifa cha Ulinzi Houssem Jbebli amesema jana kwamba hii ni baada ya operesheni ya siku nne iliyoendeshwa kati ya Septemba 15 na 18.

Amesema waliozuiwa ni pamoja na raia 581 wa Tunisia na wengine wakitokea kusini mwa jangwa la Sahara.

Vikosi vya usalama vya Tunisia vilianzisha operesheni katika maeneo mbalimbali ya pwani ambayo ni pamoja na Sfax, ambako idadi kubwa ya wahamiaji huanzia safari zao kwenda Italia.

Wiki iliyopita, Tunisia ilisema imeanzisha operesheni kubwa ya kusimamisha biashara haramu ya binaadamu na kuzuia idadi kubwa ya watu wanaokufa katika safari za mateso za baharini wakikimbilia Ulaya kutokea kwenye pwani zake.

Soma pia:

Kisiwa cha Lampedusa chashuhudia ongezeko la wahamiaji

Wahamiaji 438 waokolewa katika bahari ya Mediterania