1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi ya Tunisia yawakamata waliotoroka jela

7 Novemba 2023

Wizara ya mambo ya ndani ya Tunisia Jumanne imefahamisha kuwa vikosi vya usalama vimewakamata wafungwa watano waliopatikana na hatia kwa mashtaka ya "ugaidi" ambao pia walitoroka katika gereza la Mornaguia Oktoba 31.

https://p.dw.com/p/4YWMw
Ecuador | Gefängnisaufstände | Turi Haftanstalt in Cuenca
Picha: AFP via Getty Images

Mamlaka za Tunisia zilisema huko kutoroka kwao ilikuwa operesheni iliyopangwa kwa uangalifu.

Wizara hiyo imesema watu wanne walikuwa wamejificha kwenye mlima Boukornine", karibu kilomita 30 kusini mashariki mwa mji mkuu Tunis, huku mfungwa mwingine, Ahmed al-Malki akikamatwa Novemba 5 kwa usaidizi wa raia wa wilaya ya Ettadhamen, kitongoji chenye watu wengi cha Tunis.

Al-Malki anayefahamika kwa jina la "Al-Somali", alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 24 jela, kufuatia mauaji ya viongozi wa upinzani, akiwemo Chokri Belaid aliuawa Februari mwaka 2013, mauaji ambayo makundi ya kigaidi yalidai kuhusika na yaliyozusha mgogoro wa kisiasa nchini humo.