1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ajali ya boti yauwa zaidi ya watu 10 DRC

14 Februari 2024

Zaidi ya watu 10 wamekufa na wengine kadhaa hawajulikani walipo baada ya boti mbili kugongana kwenye mto Kongo huko magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

https://p.dw.com/p/4cMlA
Eneo la Muanda DRC
Wavuvi wakivuta nyavu zao kwa mkono kutoka ufuo wa Muanda kwenye Bahari ya Atlantiki kwenye mlango wa Mto Congo.Picha: ALEXIS HUGUET/AFP via Getty Images

Akielezea tukio hilo mmoja kati ya maafisa wa serikali katika eneo hilo, Eliezer Ntambwe amesema boti hizo mbili ambazo zilikuwa na idadi kubwa ya  mizigo na abiria ziligongana Jumatatu katika eneo la mto huo huko mashariki mwa mji mkuu, Kinshasa. Hata hivyo haijaweza pia kufahamika idadi gani ya watu imefanikiwa kuokolewa katika ajali hiyo.Vyombo vya usafiri nchini Kongo vinamilikiwa na watu binafsi, na maafisa wamekuwa wakionya kuwa hawafuati masharti ya usalama wa wasafiri. Januari ilitokea ajali ya boti ambapo watu 50 walitangazwa kupoteza maisha.