1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliokufa ajali ya mashua Mto Kongo waongezeka

17 Oktoba 2023

Idadi ya vifo kufuatia kuzama kwa boti katika Mto Kongo wiki iliyopita imeongezeka kufikia 47, huku watu wengi wakiwa bado hawajulikani waliko.

https://p.dw.com/p/4Xcqd
Demokratischen Republik Kongo | Congo River
Mto KongoPicha: Frans Lanting/picture alliance

Hayo yalisemwa na Waziri wa Usafiri wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Marc Ekila, siku ya Jumatatu (Oktoba 16).

Ripoti za awali kutoka mamlaka za jimbo la kaskazini mashariki la Equateur siku ya Jumapili (Oktoba 16) zilisema miili 28 ilikuwa imeopolewa kutoka mtoni na watu wengine kadhaa walikuwa bado hawajapatikana.

Soma zaidi: Watu 28 wafa maji Mto Kongo
Manusura waomba msaada baada ya ajali ya Meli nchini Kongo

Akizungumza na vyombo vya habari siku ya Jumatatu, Waziri Ekila alithibitisha idadi mpya ya vifo lakini akasema hawakufanikiwa kupata idadi kamili ya abiria waliokuwamo katika boti hiyo kutokana na utaratibu kukiukwa katika kuorodhesha abiria chomboni.