1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMsumbiji

Msumbuji: Raia waandamana kupinga matokeo uchaguzi

27 Oktoba 2023

Watu wawili wameuawa katika maandamano nchini Msumbuji ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa mitaa.

https://p.dw.com/p/4Y8CK
Maandamano ya raia mjini Maputo wakipinga matokeo ya uchaguzi
Maandamano ya raia mjini Maputo wakipinga matokeo ya uchaguziPicha: Marcelino Mueia/DW

Shirika lisilo la kiserikali la Centre for Public Integrity - CIP limesema polisi waliwafyatulia risasi za moto waandamanajai katika miji kadhaa.

Kundi kuu la upinzani nchini humo likiongozwa na chama cha RENAMO liliitisha maandamano baada yamatokeo ya uchaguzi wa Oktoba 11 kutolewa na maafisa wa uchaguzi Alhamisi, yakionyesha kuwa chama tawala cha Frelimo kilitangazwa mshindi katika manispaa 64 kati ya 65.

Maandamano yalipangwa katika mji mkuu Maputo na katika miji ya kaskazini ya Nacala na Nampula, huku polisi wakiwafyatulia risasi waandamanaji katika maeneo mengine.

Soma pia:Waandamanaji waingia mitaani kupinga wizi wa uchauzi Msumbiji

Taarifa ya CIP imesema polisi mmoja alidaiwa kushambuliwa na umma katika mji wa NAMPULA na kujeruhiwa vibaya na kufariki hospitalini.

Imesema mwanaume moja aligongwa na kitu kizitona kuuawa katika mji wa Nacala. Watu wengine wawili walipigwa risasi na kujeruhiwa katika maandamano ya eneo hilo.