1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamanaji waingia mitaani kupinga wizi uchauzi Msumbiji

18 Oktoba 2023

Waandamanaji wameingia mitaani nchini Msumbiji kupinga wizi wa kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na manispaa, huku polisi wakitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji hao katika mji mkuu, Maputo.

https://p.dw.com/p/4Xhcf

Huku matokeo rasmi ya mwisho ya uchaguzi wa Jumatano wiki iliyopita yakisubiriwa, chama tawala cha Frelimo kimetangazwa mshindi katika miji mingi ambako uhesabuji wa kura umekamilika.

Matokeo hayo yamepingwa na chama kikuu cha upinzani Renamo, ambacho kinadai ushindi hususan mjini Maputo.

Soma zaidi: Machafuko yaibuka Msumbiji, ikisubiri matokeo ya uchaguzi

Akiuhutubia umati wa watu mjini humo, Rais wa Renamo Ossufo Momade alitoa wito kuwataka raia wote wa Msumbiji washiriki maandamano ya kupinga udanganyifu katika uchaguzi akisema huu ni mwanzo wa mapinduzi nchini humo.