Machafuko yaibuka Msumbiji, ikisubiri matokeo ya uchaguzi
14 Oktoba 2023Matangazo
Matokeo ya awali yaliyotolewa jana Ijumaa yalionyesha kuwa chama cha upinzani Renamo kimepata zaidi ya asilimia 52 ya kura mjini Maputo, huku Frelimo ikipata chini ya asilimia 40, na hivyo kuupa upinzani ushindi ambao haujawahi kushuhudiwa.
Soma pia: Rais wa Msumbiji awatimua mawaziri sita serikalini
Chama cha upinzani cha Renamo hakijawahi kushinda uchaguzi wa katika nchi hiyo iliyopata uhuru mwaka 1975 kutoka kwa Ureno. Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa siku chache zijazo, huku tume ya uchaguzi ikisisitiza kwenye mitandao ya kijamii kwamba raia watapaswa "kuheshimu matokeo".