MigogoroUrusi
Watu 8 wauawa katika shambulizi la Urusi Kramatorsk
28 Juni 2023Matangazo
Watu wengine wasiopungua 56 walijeruhiwa katika shambulio hilo lililoulenga mgahawa huo unaotembelewa zaidi na waandishi habari, wafanyakazi wa misaada na wanajeshi wanaoutumia mji wa Kramatorsk kama kituo cha operesheni zao.
Watoto watatu ni miongoni mwa waliokufa.
Mwendesha mashtaka mkuu Andrii Kostin amesema shambulio hilo lilitokea baada ya watu kurejea kutoka kazini.
Amesema watoto watatu waliokufa walikuwa na umri wa miaka 14 na 17.
Ukraine ilianzisha operesheni yake ya kurejesha maeneo yanayoshikiliwa na Urusi mapema mwezi huu, ambayo mpaka sasa imepata mafanikio madogo.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alitangaza Jumanne kuwa vikosi vya Ukraine vimesonga mbele katika kila upande.