1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Makombora ya Urusi yailenga Kyiv na kuua watu karibu 11

13 Juni 2023

Makombora ya Urusi yamelenga majengo kadhaa ya raia katika mji wa Kryvyi Rih nchini Ukraine usiku wa kuamkia leo na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 11 na wengine chungunzima kujeruhiwa.

https://p.dw.com/p/4SWmd
Picha hii iliyopigwa na watoa huduma za Dharura kwenye jimbo la Ukraine mnamo Juni 13, 2023, inaonyesha wazima moto wakizima moto kwenye jengo la makazi la ghorofa tano, katika jiji la Kryvyi Rig, baada ya kusambuliwa na Urusi.
Urusi imeongeza mashambulizi dhidi ya Ukraine wakati jeshi la Kyiv likiwa linajiandaa na mashambulizi ya ksuhtukiza dhidi ya Urusi.Picha: AFP

Mashambulio yaliharibu maghala na majengo ya makaazi ya tu.

Mashambulio hayo yaliyofanyika mji alikozaliwa rais Volodymyr Zelensky yamekuja wakati wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika hatua za awali za operesheni yake ya kukabiliana na Urusi. Picha zilizorushwa kwenye mtandao wa Telegram wa rais Zelenksy zimeonesha jinsi zima moto wanavyopambana kuudhibiti moto ulioharibu jengo la makaazi ya raia.

Soma Zaidi:Macron, Scholz na Duda wajadili amani ya Ukraine 

Meya wa mji huo wa  Kryvi Rih Oleksandr Vilkul, amesema watu 28 wamejeruhiwa.Rais Zelensky ameandika kwenye mtandao huo wa Telegram kwamba mashammbulio hayo yamewafanya na magaidi wa Urusi.

Katika hatua nyingine, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti Nyuklia IAEA, Rafael Grossi anatarajiwa mjini Kiev leo Jumanne katika ziara ambayo amepangiwa kukutana na rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky lakini pia kutembelea kinu cha Nyuklia cha Zaporizhzhia kinachodhibitiwa na Urusi

Hatua hiyo inakuja baada ya kuharibiwa wiki iliyopita,bwawa kubwa la karibu na kinu hicho. Shirika la IAEA siku ya Jumapili  lilisema linahitaji kufika kwenye eneo hilo kutazama kiwango cha maji baada ya bwawa hilo kupoteza sehemu kubwa ya maji kutokana na uhribifu uliofanyika kwenye chanzo cha maji ya bwawa Kakhovka. Serikali ya Kiev inailaumu Urusi kwa kuhusika na uharibifu wa bwawa hilo la Kusini mwa Ukraine.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW