1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 10 wauwawa katika shambulizi la baa mashariki mwa Congo

Josephat Charo
3 Septemba 2024

Watu 10, wakiwemo raia watano na wanajeshi watano wameuliwa katika shambulizi lililofanywa kwenye baa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

https://p.dw.com/p/4kCYd
Waasi katika viunga vya mji wa Bunia, mkoani Ituri
Waasi katika viunga vya mji wa Bunia, mkoani IturiPicha: Stephen Morrison/dpa/picture alliance

Raia watano na wanajeshi watano wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameuwawa katika shambulizi lililofanywa ndani ya baa moja katika eneo linalokabiliwa na machafuko mashariki mwa nchi hiyo.

Duru za jeshi na za katika eneo hilo zinasema washambuliaji waliokuwa wamejihami na silaha waliingia ndani ya baa hiyo katika mji wa Nizi kiasi kilomita 20 kaskazini mwa mjii mkuu wa jimbo la Ituri, Bunia siku ya Jumapili jioni.

Mkuu wa jeshi la polisi wa Djugu, kanali Ruphiri Mapela ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba washambuliaji hao walimuua hapo hapo chifu wa kimila na watu wengine watatu akiwemo muwakilishi wa shirika la kijamii.

Mapela aidha amesema raia mwingine aliyepigwa risasi alikufa baada ya kukimbizwa hospitali. Kanali huyo alisema shambulizi hilo liliwafanya wanajeshi walioko Nizi kuchukua hatua ambapo watano waliuliwa.

Akithibitisha idadi ya vifo, msemaji wa jeshi ngazi ya mkoa Luteni Jules Ngongo amesema washambuliaji waliwavizia wanajeshi hao.