1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo: Kundi la M23 laua watu watano huko Masisi

16 Julai 2024

Kundi la wapiganaji wa M23 huko mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, limetuhumiwa na vyombo vya usalama kuwauwa watu watano katika mji mdogo wa Bweremana wilayani Masisi, kilometa 40 kutoka Goma.

https://p.dw.com/p/4iMLr
Uasi wa M23 Kongo
Waasi wa M23 wameendeleza mashambulizi yao mashariki ya Kongo dhidi ya raia na vikosi vya serikaliPicha: Arlette Bashizi/REUTERS

Vyanzo vya ndani vimeeleza kuwa M23 walivurumisha mabomu mawili kwenye eneo hilo na kusababisha pia uharibifu mkubwa ikiwemo vifo vya raia hao. Vyanzo hivyo, vimesema  kuwa tangu asubuhi ya Jumanne, kumekuwa na hali ya wasiwasi kwenye eneo hilo wakati mapigano yakiendelea kwenye vijiji vya Kashingamutwe na Ndumba.

Soma pia: Wakongomani hawajafikiwa na misaada licha ya usitishwaji vita

Mnamo Julai 4, Marekani ilipendeleza kuwepo kwa makubaliano ya wiki mbili ya usitishwaji mapigano kwa sababu za kibinadamu kote mkoani Kivu kaskazini, mkataba ambao umekiukwa na pande zote mbili kwenye mzozo huo.