1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wastaafu Tanzania wafurahishwa na kikokotoo kipya

Admin.WagnerD27 Mei 2022

Baada ya Tanzania kupandisha hadi asilimia 33 kiwango cha kukokotoa mafao ya mkupuo kwa wafanyakazi waliostaafu kumekuwa na hisia mseto, wapo wanaosema wamefurahishwa na hatua hiyo ya serikali.

https://p.dw.com/p/4Bwjz
Tansania | Teilnehmer am 58. Jahrestag der Gewerkschaft in Dodoma
Picha: Ericky Boniphace

Kabla ya hatua hiyo ya serikali ya Tanzania, wafanyakazi waliostaafu walikuwa wakipewa asilimia 50 ya fedha za awali pindi wanapostaafu.

Baada ya kufanyika kwa  mabadiliko yakanuni ya kukokotoa mafao ya mwaka 2018 yalipendekeza kiwango hicho kupunguzwa hadi asimilia 25, jambo ambalo lilizua mjadala mkubwa.

 Uamuzi wa sasa wa kuwapatia wastaafu asilimia 33 ya fedha ya kiinua mgongo ilipokelewa kwa hisia mseto na baadhi ya wafanyakazi waliostaafu katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Abdallah Kizota aliiambia Dw kwamba, hatua ya serikali kuongeza mafao kwa wastaafu ni hatua ambayo wengi waliisubiri ukizingatia mfumo wa bei unashuhudiwa walau mafao hayo yataleta ahueni.

Soma pia:Tanzania:Kuchukua hatua kukabiliana na hali ngumu ya maisha

"inapendeza sana pale unapomaliza kulitumikia taifa kisha unapata kiinua mgongo ambacho kitakusaidia" alisema Abdallah ambae alikuwa mtumishi wa serikali katika bodi ya pambana.

TUKTA: Yawatoa wasiwasi watumishi

Hatua hiyo ya kutangazwa kiwango kipya cha kikokotoo cha mafao ya mkupuo ilifikiwa baada ya makubaliano kati ya Serikali, Chama cha Waajiri Nchini (ATE) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) baada ya kusitishwa kwa kanuni zilizotengenezwa mnamo Desemba 28 mwaka 2018.

Afrika Tansania Finanzminister  Mwigulu Nchemba
Mwandishi wa DW Dodoma Deokaji Makomba akitzungumza na waziri wa fedha Tanzania Dr.Mwigulu NchembaPicha: Deo Kaji Makomba/DW

Licha ya Shirikisho la wafanyakazi kushirikishwa katika mchakato mzima wa kutengeneza kikokotoo hicho, bado kuna wafanyakazi hawakufurahishwa na hatua hiyo.

Miongoni mwa wengi ambao hawakufurahishwa wamekuwa na wasiwasi na kuhitaji ufafanuzi zaidi wa namna kikokotoo hicho kinavyofanya kazi katika mafao ya kiinua mgongo kadhalika yale ya kila mwezi.

Soma pia:Tanzania kukopa Benki ya Dunia, IMF kupunguza bei za mafuta

Katibu mkuu wa Shirikisho la wafanyakazi nchini Tanzania, TUKTA, Kheri Mkunda aliiambia DW kwamba hakuna haja kwa wastaafu au watumishi wanaotarajiwa kustaafu kupata wasiwasi kwani wamewakilishwa vema katika zoezi hilo.

"Wale waliokuwa wakipata asilimia hamsini ya mafao kwa kila mwezi yataongezeka, lakini kile kiinua mgogo kitapungua" alifafanua na kuongeza kwamba kama shirikisho wanaona ni hatua nzuri iliofikiwa.

Tangazo hilo la kikokotoo kipya cha mafao ya mkupuo kwa wafanyakazi waliostaafu nchini Tanzania, lilitolewa Mei 26 na Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Profesa Jamal Katundu.

Alisema kuwa mshahara wa kukotolea mafao ya pensheni utakuwa wastani wa mishahara bora ya miaka mitatu ndani ya miaka 10 kabla ya kustaafu na kwamba umri wa kustaafu kwa lazima utaendelea kuwa miaka 60. Kikotoo hicho kitaanza kutumika Julai Mosi mwaka huu.

Madhila ya kazi za majumbani katika mataifa ya Kiarabu