1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTONMarekani haina mipango ya kuifunga jela ya Guantanamobay,Cuba

13 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF3r

Makamu wa rais wa Marekani Dick Cheney amesema Marekani haina mipango ya kuifunga jela ya Guantanamo Bay huko Cuba.

Marekani inawazuilia zaidi ya washukiwa wa ugaidi 500 kutoka nchi 40 kwenye jela hiyo.

Matamshi ya bwana Cheney yamekuja baada rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter kutaka jela hiyo ifungwe kufuatia shutuma zilizotolewa na makundi ya kutetea haki za binadamu juu ya kuteswa kwa wafungwa katika jela hiyo.