1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WARSAW. Mashambulio ya kulipizana kisasi yatokea

12 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CElZ

Rais Alexsander Kwasniewski wa Poland amemtaka mwenziwe rais wa Urusi Vladmir Puttin achukue hatua za kusimamisha mfululizo wa mashambulio ya wananchi wa Poland mjini Moscow Urusi.

Rais Alexsandar ametoa ombi hilo siku moja baada ya mwanahabari mmoja wa Kipoland kushambuliwa katika mji wa Moscow.

Kisa kingine kama hicho kilitokea wiki iliyopita ambapo mwanadiplomasia wa ubalozi wa Poland na mfanyakazi mmoja vile vile walishambuliwa.

Balozi wa Poland nchini Urusi Stefan Meller amewaonya wafanyakazi wa ubalozi wake dhidi ya kutembea peke yao.

Mashambulio hayo ni ishara ya kulipiza kisasi kwa kupigwa watoto wanne wa Kirusi mjini Warsaw.