1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waokoaji waendelea kufukua waliokwama Uturuki na Syria

14 Februari 2023

Timu ya uokozi inaendelea kutafuta miili na manusura zaidi chini ya vifusi katika mikoa mitatu iliyopigwa na tetemeko la ardhi wiki iliyopita nchini Uturuki na Syria.

https://p.dw.com/p/4NSDy
Türkei Syrien Erdbeben
Picha: Hiroto Sekiguchi/AP/picture alliance

Idadi ya vifo vilivyotokana na matetemeko hayo mawili yaliyokuwa na ukubwa wa 7.8  na 7.5 katika kipimo cha Richter imepindukia watu 37,000,

Hata hivyo vifo zaidi vikitarajiwa kuripotiwa kufuatia timu hiyo ya waokoaji kuendelea na operesheni yao siku ya nane baada ya janga hilo. 

Soma pia:Juhudi zahamia kwa manusura huku vifo vya tetemeko Uturuki na Syria vyapindukia 35,000

Wataalamu wanasema kuna nafasi ndogo ya kuwapata manusura, baada ya siku nyingi kupita na huenda operesheni hiyo ikasitishwa hivi karibuni