1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN:Juhudi za uokozi Uturuki na Syria zakaribia mwisho

14 Februari 2023

Umoja wa Mataifa umesema jana kuwa juhudi za uokozi kufuatia matetemeko ya ardhi nchini Uturuki na Syria zinakaribia mwisho.

https://p.dw.com/p/4NRs6
Türkei Antakya | Rettungsarbeiten nach Erdbeben
Picha: Bernat Armangue/AP Photo/picture alliance

Mkuu wa misaada wa umoja huo Martin Griffiths, alitoa kauli hiyo wakati wa ziara kwenye mji ulioharibiwa wa Aleppo, kaskazini mwa Syria.

Griffiths amesema jukumu kuu kwa sasa ni kutafuta hifadhi, chakula, uangalizi na shule kwa ajili ya waliookolewa.

Amesema msaada wa Umoja wa Mataifa sasa utatoka kwenye maeneo yanayodhibitiwa na serikali ya Syria kwenda maeneo yanayoshikiliwa na waasi kaskazini-magharibi.

Soma pia:Umoja wa Mataifa: Shughuli za uokozi zinakaribia kumalizika Uturuki, Syria

Mkuu huyo wa misaada wa Umoja wa Mataifa aliongeza kuwa dunia imeshindwa kutoa msaada wa kutosha kwa Syriakufuatia matetemeko hayo, na kusema Wasyria wanajihisi kwa usahihi kutelekezwa.

Matamshi hayo yanakuja wakati takwimu za karibuni zaidi zinaonesha idadi ya vifo kutokana na matetemeko hayo imepindukia 35,000.

Wiki moja baada ya matetemeko hayo, waokoaji wanaendelea kuwatoa manusura kwenye vifusi.