1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wawili wahukumiwa kifo kwa uoga nchini Congo

6 Julai 2024

Wanajeshi wawili wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamehukumiwa kifo siku ya Ijumaa kwa uoga na kukimbia adui ikiwa ni siku mbili tu baada ya hukumu sawa na hiyo kutolewa kwa wanajeshi 25 mashariki mwa nchi hiyo

https://p.dw.com/p/4hxhG
DRC
Mahakama nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imewahukumu hukumu ya kifo wanajeshi wawili kwa uoga na kukimbia aduiPicha: Pond5/IMAGO

Wanajeshi wawili wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamehukumiwa kifo siku ya Ijumaa kwa uoga na kukimbia adui ikiwa ni siku mbili tu baada ya hukumu sawa na hiyo kutolewa kwa wanajeshi 25 mashariki mwa nchi hiyo.

Shirika la habari la Ufaransa AFP limeripoti hukumu hizo zinatolewa wakati ambapo waasi wa M23, ambao serikali ya mjini Kinshasa inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono, wakiliteka eneo jipya la eneo la kaskazini wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Soma zaidi. Waasi wa M23 wauteka mji wa Kanyabayonga

Wanajeshi wengine wanaoshtakiwa wanatarajiwa kupandishwa kizimbani leo.

Upande wa utetezi umelaani hukumu hiyo na kutangaza nia yake ya kukata rufaa kama ilivyokuwa siku ya Jumatano ambapo askari 25 walihukumiwa kifo katika kesi iliyosikilizwa katika kijiji cha Alimbongo. Askari wengine wanane walihukumiwa kifo huko Goma mwezi Mei kwa kosa la "kuwakimbia adui.