1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waliokufa kwa maporomoko ya ardhi India wafikia 27

23 Julai 2023

Idadi ya watu waliokufa katika maporomoko makubwa ya ardhi katika jimbo la Maharashtra nchini India imeongezeka na kufikia 27, huku watu wengine takribani 50 hawajulikani walipo.

https://p.dw.com/p/4UHT4
Mvua kubwa zinazonyesha India zimesababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi
Mvua kubwa zinazonyesha India zimesababisha mafuriko na maporomoko ya ardhiPicha: Ab Rauoof Ganie/DW

Maporomoko hayo yalisababishwa na mvua za masika zilizoanza tangu siku ya Alhamis. Timu za waokoaji wa dharura zimekuwa zikichimba chini ya vilima vya ardhi na vifusi ili kutafuta miili ya waathirika.

Soma zaidi: Watu 29 wapoteza maisha kutokana na mafuriko huko India

Hata hivyo zoezi hilo linakwenda taratibu kutokana na mvua kuendelea kunyesha na uhaba wa vifaa vizito vya kuokolea. Afisa mmoja mkuu wa wilaya alisema hana matumaini ya kupata manusura katika siku ya nne ya uokoaji unaoendelea.

India imekumbwa na mvua, mafuriko na maporomoko ya ardhi tangu kuanza kwa msimu wa masika mwezi Juni na kusababisha vifo vya watu wengi.