1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu milioni moja wakimbia mafuriko India

21 Agosti 2018

Watu zaidi ya milioni moja wamejihifadhi katika kambi za muda ili kuepuka mafuriko ambayo yamewaua zaidi ya watu 410 katika jimbo la kusini magharibi mwa India la Kerala. Nyumba 50,000 zimeharibiwa vibaya.

https://p.dw.com/p/33SXD
Monsun in Indien Überschwemmungen in Kerala
Picha: picture-alliance/dpa/AP/A. Rahi

Watu wanazidi kukimbilia katika makambi wakati kiwango cha uharibifu kikionekana kutokana na maji kuanza kupungua. Miili mingine sita ilipatikana jana  Jumatatu na kufanya jumla ya idadi ya watu waliofariki kufikia 410 tangu msimu wa masika ulipoanza mwezi Juni. Timu za wanajeshi zimesema watu elfu kadhaa katika mji huo wamebaki katika nyumba zilizoharibiwa na mvua za siku kumi ambazo zimelikumba jimbo hilo. Maelfu ya wanajeshi wa kitengo cha wanamaji na anga wamesambaa maeneo yote ya jimbo hilo ili kuwasaidia wale waliokwama katika maeneo ya ndani ndani na milimani. Helikopta na ndege zisizo na rubani zinafanya kazi ya kudondosha vyakula, madawa na maji katika vijiji  ambako  mawasiliano yamekatika.

 

Baba na mwanae wakikimbia mafuriko
Baba na mwanae wakikimbia mafuriko Picha: picture-alliance/dpa/AP/A. Rahi
Nyumba nyingi zimeathiriwa na mafuriko
Nyumba nyingi zimeathiriwa na mafurikoPicha: Getty Images/A. Loke
Misaada inaanza kupelekwa kwa walioko kwenye kambi za hifadhi
Misaada inaanza kupelekwa kwa walioko kwenye kambi za hifadhiPicha: Getty Images/AFP/M. Kiran
Wanajeshi wanapeleka misaada kwa watu wanaoshindwa kuondoka kwenye nyumba zao
Wanajeshi wanapeleka misaada kwa watu wanaoshindwa kuondoka kwenye nyumba zaoPicha: picture-alliance/AP Photo