1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 29 wapoteza maisha kutokana na mafuriko huko India

10 Julai 2023

Watu 29 wamepoteza maisha baada ya siku kadhaa za kunyesha mvua kubwa za msimu kaskazini mwa India ambazo zimesababisha kukataka kwa njia za mawasiliano muhimu

https://p.dw.com/p/4TgjL
India, mafuriko
Raia akipita kwenye mafuriko huko IndiaPicha: Sri Loganathan/ZUMA Press Wire/picture alliance

Watu 29 wamepoteza maisha baada ya siku kadhaa za kunyesha mvua kubwa za msimu  kaskazini mwa India ambazo zimesababisha kukataka kwa njia za mawasiliano muhimu.India yakumbwa na janga kubwa la kibinaadamu kutokana na mafuriko

Picha za televisheni zimeonesha mafuriko makubwa na maporomoko ya udongo yakisomba magari, kuharibu majengo na kuvunja madaraja kwenye jimbo la milimani la Himachal Pradesh ambalo ndiyo limeathirika zaidi.

Vifo vingi vimetokea kwenye jimbo hilo la vingine vimeripotiwa katika majimbo ya Rajasthan, Uttar Pradesh na mikoa iliyo kwenye safu za milima ya Himalaya ya Uttarakhand na Kashmir.

Soma: Watu milioni moja wakimbia mafuriko India

Waziri Kiongozi wa jimbo la Himachal Pradesh, Sukhvinder Singh, amesema masikitiko makubwa kwa vifo vilivyotokea na kusema serikali inafanya kila juhudi za kuwasaidia watu waliokwama na walipoteza makaazi.