1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakazi wakimbia, waasi wa M23 wakiusogelea zaidi mji wa Goma

31 Mei 2024

Wakaazi wa mji wa Goma nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameanza kukimbia wakati ambapo waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wakiwa wanaujongelea mji huo muhimu wa mashariki.

https://p.dw.com/p/4gUF8
DR Kongo | Shambulizi katika kambi la Bulengo, mjini Goma
Picha hii ilipigwa Mei 6, 2024 baada ya makazi za wakimbizi wa ndani kushambuliwa Mei 3, 2023Picha: Aubin Mukoni/AFP/Getty Images

Afisa mmoja wa serikali amenukuliwa akisema kuwa waasi wa M23 wanaukaribia mji wa Kanyabayonga uliopo kwenye njia inayoelekea katika mji wa Goma.

Kwa mujibu wa taarifa, mapigano yametokea kwenye eneo la Masisi karibu na mji wa Sake uliopo umbali wa kilometa 20 kutoka Goma.

Majeshi la serikali ya Kongo yamejaribu kuwarudisha nyuma waasi hao wa M23 wanaosemekana kuwa wameuzingira mji wa Goma ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.