Wahouthi waelekea Saudi Arabia kwa mazungumzo ya amani Yemen
15 Septemba 2023Ujumbe wa waasi hao wa kihouthi wenye uhusiano wa Karibu na Iran ambayo ni hasimu wa muda mrefu wa Saudi Arabia, uliondoka jana jioni kwa ziara yao ya kwanza ya wazi tangu muungano unaoongozwa na Saudi Arabia, ulipoiingilia kijeshi Yemen mwaka 2015.
Ziara ya waasi hao ni ishara ya matumaini ya hivi karibuni ya kusitisha mapigano yaliyosababaisha mgogoro mkubwa na mbaya wa kibinaadamu nchini humo.
Kiongozi wa juu wa kisiasa wa kundi hilo Mohamed Ali al-Huthi aliandika katika mtandao wa X uliokuwa Twitter zamani, kwamba anatumai kutakuwa na majadiliano muhimu kwa manufaa ya watu wote na kwamba changamoto zilizopo zitatatuliwa. Amesema mazungumzo yanaweza tu kufanyika chini ya muungano huo akitilia maanani kwamba uamuzi wa mzingiro na kuusimamisha uko mikononi mwa muungano huo.
Waasi wa Huthi wanaoungwa mkono la Iran kwenda Saudi Arabia
Kipengee muhimu cha kupunguza uhasama ni kurejea kwa mahusiano mazuri kwa Saudi Arabia na Iran waliokuwa maadui wa muda mrefu.
Marekani yapongeza juhudi za kutafuta amani ya Yemen
Marekani mshirika wa Saudi Arabia imepongeza ziara ya Wahouthi ikisema kusitisha vita vya Yemen ni moja ya vipaumbele vya sera ya kigeni ya rais Joe Biden. Mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani Jake Sullivan amesema nchi yake imetoa mwito kwa pande zote husika katika vita hivyo, kuangalia mafanikio ya kusitisha mapigano kwa watu wa Yemen.
Televishani ya kitaifa ya Saudi Arabia imesema mazungumzo ya sasa yanalenga kupata suluhu ya kudumu ya mkwamo wa kisiasa yemen yatakayoioandoa nchi hiyo kutoka hali ya mgogoro had uthabiti wa kweli.
Yemen: Baraza jipya la Aden na hatari ya mzozo na wanaoungwa mkono na UAE
Miongoni mwa matakwa ya wahouthi ni wafanyakazi wa umma kulipwa mishahara yao na serikali ya Yemeni na kuanzishwa kwa safari nyengine za ndege katika maeneo mapya kutoka uwanja wa ndegee wa sanaa.
Yemen iliingia katika mgogoro wakati waasi wa Houthi walipoudhibiti mji mkuu Sanaa mwezi September mwaka 2014 na kuiondoa madarakani serikali iliyokuwa inatambuliwa kimataifa, hali iliyosababisha Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudia kuanzisha operesheni ya kijeshi mwezi Machi mwaka 2015.
Mapigano ya Yemen yamesababisha mauaji ya maelfu ya watu na kuwalazimisha wengine kuyahama makaazi yao ikiacha thuluthi tatu ya idadi ya watu wakitegemea misaada ya kiutu.
afp/ap