1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa Huthi wanaoungwa mkono la Iran kwenda Saudi Arabia

14 Septemba 2023

Ujumbe wa waasi wa Kihuthi wanaoungwa mkono na Iran unatarajiwa kwenda Saudi Arabia, ikiwa ni ziara ya kwanza hadharani tangu muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ulipoanzisha mapigano dhidi yao mwaka 2015.

https://p.dw.com/p/4WLaC
Baadhi ya maafisa wa Saudi arabia,Yemeni na Omani wakiwa katika picha ya pamoja na waasi wa Houthi
Baadhi ya maafisa wa Saudi arabia,Yemeni na Omani wakiwa katika picha ya pamoja na waasi wa HouthiPicha: Ansar Allah Media Office/AP/picture alliance

Duru zinazohusika na mazungumzo hayo zimesema,wajumbe kutoka kundi la Kihuthi na kutoka Oman wanakwenda nchini humo kwa mazungumzo ya kujaribu kujadiliana juu ya kusitisha moja kwa moja mapigano ili hatimaye kuvimaliza vita nchini Yemen.

Mwanadiplomasia mmoja wa magharibi nchini Yemen, amethibitisha juu ya ziara hiyo, akisema ujumbe huo unaweza kwenda leo ama siku mbili zijazo.

Soma pia:Je makubaliano ya kusitisha mapigano Yemen yatafanikiwa?

Mjumbe wa baraza la kisiasa la Huthi Ali Al-Qhoom pia ameitangaza ziara hiyo kupitia mtandao wa X, ingawa maafisa wa Saudi Arabia hawajazungumzia chochote.

Yemen, ilitumbukia katika vita baada ya Huthi kudhibiti mji mkuu SanaaSeptemba 2014, hatua iliyoingiliwa kati na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia.