1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Waasi wa Huthi wawauwa wanajeshi 10 wa Yemen

27 Agosti 2023

Waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran wamewauwa wanajeshi 10 wa jeshi la Yemen kutoka kundi linalotaka kujitenga kusini mwa nchi hiyo, katika "shambulizi la kushtukiza".

https://p.dw.com/p/4VciM
Pichani ni mmoja ya wakaazi akikagua uharibifu uliosababishwa na shambulizi la vikosi vinavyoongozwa na Saudi Arabia na kulenga ngome za waasi wa Huthi, Januari 18,2022
Yemen imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi yaliyosababisha uharibifu mkubwa wa hata makaazi ya watu.Picha: Mohammed Huwais/AFP/Getty Images

Shambulizi hili linafanyika baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa utulivu nchini humo.

Duru za kijeshi zimeliambia shirika la habari la AFP kwamba wanajeshi wengine 12 walijeruhiwa katika shambulizi hilo lililofanywa katika mpaka kati ya mikoa ya kusini ya Lahj na Al-Bayda.

Wapiganaji wanne wa Houthi pia waliuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Hakukuwa na tamko lolote lililotolewa kutoka kwa waasi hao.

Shambulizi hilo lililenga eneo linalodhibitiwa na waasi hao wanaotaka kuunda Yemen Kusini huru sawa na serikali iliyokuwepo hadi 1990.

Soma Pia: Saudi Arabia na Wahouthi watafuta suluhu Yemen