1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafungwa zaidi ya 22 elfu wameachiwa huru nchini Rwanda

23 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEid

Wafungwa 22400 wameachiwa huru mwishoni mwa mwezi uliopita nchini Rwanda.Habari hizo zimetangazwa na katibu mkuu wa wizara ya sheria Johnson Busingye mjini Kigali. Wafungwa 36 elfu walikua waachiliwe huru hapo awali.Kwa mujibu wa wizara ya sheria,hadi mwisho wa mwezi July uliopita,jela za Rwanda zilikua zimeshenei wafungwa 82 elfu,wengi wao wanatuhumiwa kuhusika na mauwaji hayo ya halaiki ya mwaka 1994..Mpango wa kuwaachia huru wafungwa unafuatia amri ya rais Paul Kagame,aliyewataka january mosi mwaka 2003,madhamana waachie huru kwa muda baadhi ya wafungwa waliokiri madhambi yao..Mpango huo umepelekea zaidi ya watu 22 elfu kuachiwa huru mwaka 2003 na wengine 2400 mwaka Wafungwa 22400 wameachiwa huru mwishoni mwa mwezi uliopita nchini Rwanda.Habari hizo zimetangazwa na katibu mkuu wa wizara ya sheria Johnson Busingye mjini Kigali. Wafungwa 36 elfu walikua waachiliwe huru hapo awali.Kwa mujibu wa wizara ya sheria,hadi mwisho wa mwezi July uliopita,jela za Rwanda zilikua zimeshenei wafungwa 82 elfu,wengi wao wanatuhumiwa kuhusika na mauwaji hayo ya halaiki ya mwaka 1994..Mpango wa kuwaachia huru wafungwa unafuatia amri ya rais Paul Kagame,aliyewataka january mosi mwaka 2003,madhamana waachie huru kwa muda baadhi ya wafungwa waliokiri madhambi yao..Mpango huo umepelekea zaidi ya watu 22 elfu kuachiwa huru mwaka 2003 na wengine 2400 mwaka jana.Wengi kati ya walioachiwa huru kwa muda watabidi kupita katika mahakama za kienyeji „Gacaca“ kujibu madai ya kuhusika na mauwaji ya halaiki.