1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Haki za binadamuAfghanistan

Vizuizi dhidi ya wanawake vyazidi kuitenga Afghanistan

22 Juni 2024

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa amesema vizuizi dhidi ya haki za wanawake vinaendelea kuizuia Afghanistan kujumuishwa kwenye jumuiya ya kimataifa.

https://p.dw.com/p/4hNef
Mwanamke wa Afghanistan akiwa amevaa Burqa
Mwanamke wa Afghanistan akiwa kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani iliyopo kwenye viunga vya Kabul, Disemba 27, 2012. Wanawake nchini humo wanadhibitiwa na sheria kali ikiwa ni pamoja na za mavaziPicha: SHAH MARAI/AFP via Getty Images

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNAMA Roza Otunbayeva amelimbia Baraza la Usalama kwamba vizuizi kwa wanawake na wasichana haswa katika elimu vimeendelea kuligharimu taifa hilo na kudhoofisha mustakabali wake.

Amesema vizuizi hivyo pia vinaondoa uaminifu juu ya uhalali wa vizuizi hivyo unaodaiwa na mamlaka ya nchini humo ya Taliban, ambao kulingana na afisa huyo inaendelea kuzuia suluhu za kidiplomasia zitakazoisaidia Afghanistan kuunganishwa tena kwenye jumuiya ya kimataifa.

Tangu waliporejea madarakani mwaka 2021, mamlaka ya Taliban haijatambuliwa rasmi na taifa lolote na imekuwa ikitumia sheria kali ya Uislamu, kukandamizwa uhuru wa wanawake unaotajwa na Umoja wa Mataifa kama "ubaguzi wa kijinsia."