1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Taliban: Mwanamke anashuka thamani akiacha wazi uso wake

18 Agosti 2023

Kundi la Taliban lawahimiza wanawake nchini Afghanistan kufunika nyuso akiwa nje ya nyumba.

https://p.dw.com/p/4VJIi
Taliban ladai ikiwa nyuso za wanawake zitaonekana hadharani kuna uwezekano wa kusababisha fitina.
Taliban ladai ikiwa nyuso za wanawake zitaonekana hadharani kuna uwezekano wa kusababisha fitina.Picha: Tolo TV/DW

Msemaji wa wizara muhimu katika serikali ya Taliban huko Afghanistan amesema wanawake hupoteza thamani ikiwa wanaume wataweza kuziona nyuso zilizofunuliwa hadharani.

Ameongeza kuwa, kidini wasomi nchini humo wanakubaliana kwamba mwanamke lazima afunike uso wake akiwa nje ya nyumba.

Molvi Mohammad Sadiq Akif, msemaji wa Wizara ya Taliban yenye kuhusika na masuala ya jamii amesema ikiwa nyuso za wanawake zitaonekana hadharani kuna uwezekano wa kusababisha fitina, au kuanguka katika dhambi.

Taliban, iliyopata dhamana ya nchi Agosti 2021, wanaonekana kama wenye kushindwa kutoa muongozo sahihi wa kuvaa hijab, ikiwa pia ni sababu ya kuwazuia wanawake kujitokeza katika maeneo ya wazi kama ya bustani, kushiriki kazi na chuo kikuu.