1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Visa vya utekaji nyara vyaripotiwa nchini ethiopia

9 Julai 2024

Balozi wa Marekani nchini Ethiopia amesema takriban watu 100 wakiwemo wanafunzi walitekwa nyara wiki iliyopita katika maeneo yanayokabiliwa na mapigano katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia.

https://p.dw.com/p/4i4c8
alozi wa Marekani nchini Ethiopia Ervin Massinga
Balozi wa Marekani nchini Ethiopia Ervin MassingaPicha: Seyoum Getu/DW

Utekaji nyara huo umekuwa ukifanywa na watu wanaodai kulipwa kigombozi.

Balozi huyo wa Marekani, Ervin Massinga ameandika kupitia ukurasa wa x akisema matukio hayo ya mara kwa mara ya hivi karibuni katika majimbo yaOromia na Amhara yanaonesha ni kwa jinsi gani mgogoro uliochukuwa muda mrefu kumalizika,ulivyotanuwa visa vya uhalifu na kudhoofisha  utawala wa sheria.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW