1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vatican. Idara ya Uislamu yarejeshewa hadhi yake.

29 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxB

Kiongozi wa kanisa Katoliki Pope Benedict 16 ameamua kurejesha katika makao makuu ya utawala wake , idara ambayo inaangalia mdahalo na dini ya Kiislamu katika hadhi yake ya pekee ya hapo mwanzo.

Benedict aliishusha idara hiyo March 2006 kwa kuiweka pamoja na wizara ya utamaduni katika Vatican.

Maafisa wa Kikatoliki na Kiislamu wamesifu uamuzi huo kuwa ni hatua muhimu ambayo inaweza kusaidia kuimarisha uhusiano baina ya kanisa Katoliki na Uislamu.

Mdahalo baina ya Ukatoliki na Uislamu bado unaendelea kuathirika kutokana na athari mbaya zilizotokana na hotuba iliyotolewa na kiongozi huyo wa kidini katika mji wa Ujerumani wa Regensburg mwaka jana. Baadaye aliomba radhi kwa kutofahamika na Waislamu, lakini mahusiano yamebaki kuwa mabaya.