1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya waridhia vikwazo vipya dhidi ya Urusi

24 Juni 2024

Mataifa ya Umoja wa Ulaya yameridhia juu ya nyongeza ya vikwazo vipya dhidi ya Urusi kutokana na vita vyake nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4hQmv
Brussels | Mkutano wa wafadhili wa Syria
Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Espen Barth Eide, wa pili kushoto, akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan, Ayman Safadi, wa pili kulia, wakati wa mkutano kwenye jengo la Baraza la Ulaya mjini Brussels, Mei 27, 2024.Picha: Geert Vanden Wijngaert/AP Photo/picture alliance

Ngwe hii ya 14 ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Urusi ni pamoja na kupiga marufuku uingizwaji upya gesi asiliaya kimiminika ya Urusi katika mataifa ya Umoja wa Ulaya kwa kutumia mataifa ya nje ya umoja huo.

Kadhalika unatoa vitendea kazi zaidi katika kukabiliana na ukwepaji wa vikwazo, pamoja na kulenga nyongeza ya watu 116 binafsi na taasisi nyingine zenye kushiriki hatua ovu dhidi ya Ukraine.

Hatma ya mali ya Urusi iliyouzuilwa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji Hadja Lahbob ni anazungumzia mazli za Urusi zilizozuiliwa "Kwa zingatio la mali za urusi zilizozuiliwa, kuna makubaliano, tulifanikiwa kufikia mchakato huo ili kuwa na dhamana inayohitajika na kuruhu faida kutoka katika mali hizo za Urusi zilizozuiliwa."

Mzima moto wa Ukraine huko Zaporizhzhia
Shambulio la kombora la Urusi huko Zaporizhzhia. Urusi ilifanya shambulio lingine kubwa la ndege zisizo na rubani na kombora dhidi ya miji ya Ukraine usiku wa Machi 22, ikilenga Kharkiv, Zaporizhzhia na Kryvyi.Picha: Andriy Andriyenko/SOPA Images/picture alliance

Katika hatua nyingine Waziri wa Mambo ya Nje wa Lithuania Gabrielius Landsbergis ameutaka Umoja wa Ulaya kuchukua hatua za ziada katika kukabiliana na vitendo vinavoshamiri vya Urusi kufanya mashambulizi katika katika mataifa ya Umoja wa Kujihami wa NATO.

Kitisho cha mashambulizi ya Urusi kwa mataifa ya NATO

Akizungumza kabla ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa umoja huo wa huko Luxenbourg, Waziri Landsbergis amesema lazima wawe wazi zaidi katika kutafuta namna ya kupata ufumbuzi wa jambo hilo, ingawa pia aliongeza kuwa kwa bahati mbaya hadhani kama kuna uwajibikaji katika katika suala hilo.

Na Idadi ya vifo vilivyotokana na mashambulizi ya Jumapili katika eneo la kusini mwa Urusi la Dagestan yameongezeka hadi kuifikia watu 19. Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa kamati ya uchunguzi ya Urusi.

Aidha, katika taarifa hiyo, ambayo imetolewa leo hii kamati hiyo imesema, washambuliaji watano pia waliwawa wakati wa makabiliano ya mashambulizi.

Soma zaidi:Mashambulizi ya Urusi yawauwa watu wawili mjini Kharkiv

Taarifa hiyo imethibitishwa na Gavana wa mkoa huo Sergei Melikov alieeleza kuwa watu wenye silaha walishambulia kwa risasi makanisa mawili ya Kiorthodox, sinagogi na vituo vya polisi katika miji miwili ya Derbent na Makhachkala.

Awali Wizara ya Mambo ya Ndani ya  Dagestan ilesema kundi la watu wenye silaha lilifanya mashambulizi hayo karibu wakati mmoja na kwamba kanisa na sinagogi vyoote viliteketea kwa moto.

Ndani nchini Ukraine makombora ya Urusi yaliolenga mji wa kusini mwa Ukraine wa Odesa yamebomoa jengo na kuwajeruhi watu watatu, akiwemo kijana wa umri wa miaka 19. Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa gavana wa mkoa huo Ole Kiper. Jengo lililoshambuliwa lilikuwa na jumla ya watu 50 wakifanya kazi kwa wakati huo.

Chanzo: RTR/AFP