1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mashambulizi ya Urusi yawauwa watu wawili mjini Kharkiv

Sylvia Mwehozi
22 Juni 2024

Mashambulizi ya Urusi katika mji wa kaskazini mashariki mwa Ukraine wa Kharkiv yamewaua watu wawili na kujeruhi wengine 15 siku ya Jumamosi.

https://p.dw.com/p/4hOGS
Ukraine | Mwanajeshi
Askari wa UkrainePicha: Pablo Miranzo/Anadolu/picture alliance

Mashambulizi ya Urusi katika mji wa kaskazini mashariki mwa Ukraine wa Kharkiv yamewaua watu wawili na kujeruhi wengine 15 siku ya Jumamosi. Kulingana na gavana wa eneo hilo Oleg Synegubov, askari wa Urusi walishambulia jengo la makazi kwa mabomu mchana wa Jumamosi.Uholanzi yatangaza kuisaidia Ukraine mfumo wa kujilinda angani

Kharkiv, mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine, uko karibu na mpaka wa Urusi na umeharibiwa vibaya katika mashambulizi ya mara kwa mara.  Urusi ilianzisha mashambulizi mapya katika eneo la Kharkiv mnamo mwezi Mei, na kupata mafanikio makubwa zaidi katika eneo hilo kwa muda wa miezi 18.

Awali, Urusi ilifyatua mkururo wa makombora na droni usiku wa kuamkia leo nchini Ukraine na kuharibu miundombinu ya nishati upande wa kusini mashariki na magharibi na kuwajeruhi wafanyakazi wawili.