1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUholanzi

Uholanzi yatangaza kuipatia Ukraine mfumo wa kujilinda

22 Juni 2024

Waziri wa Ulinzi wa Uholanzi Kajsa Ollongren ametangaza jana kwamba taifa hilo pamoja na nchi nyingine wataipatia Ukraine mfumo wa ziada wa ulinzi wa angani wa Patriot, limesema shirika la habari la Uholanzi ANP.

https://p.dw.com/p/4hNee
Uholanzi kuipatia Ukraine mfumo wa kujilinda
Waziri wa Ulinzi wa Uholanzi Kajsa Ollongren akisalimiana na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine wakati wa ziara kwenye kambi ya Soesterberg Mei 4, 2023Picha: Yves Herman/AP/picture alliance

Ollongren amesema nchi hiyo nyingine itatoa taarifa yenyewe. Uholanzi itatoa mfumo wa pili wa Patriot kwa Kiev wiki hii, baada ya kukabidhiwa mfumo mwingine na Romania.

Mwishoni mwa mwezi Mei, serikali ya Uholanzi ilitangaza kutoa mfumo huo wa kujilinda.

Ollongren aidha aliwaomba washirika wa Umoja wa Ulaya kutoa vifaa kwa ajili ya mfumo huo ambao ndio pekee wa kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Urusi.